APIGWA RISASI AKITAFUNA USO WA MWENZAKE HADHARANI...
http://roztoday.blogspot.com/2012/05/apigwa-risasi-akitafuna-uso-wa-mwenzake.html
Tukio la polisi kumpiga risasi na kufa mtu aliyekuwa kitafuna uso wa mwenzake huku akiwa uchi limenaswa kwenye kamera za CCTV.
Picha hizo zinaonesha miguu ya wanaume wawili ikichomoza kwenye daraja la waenda kwa miguu mjini Miami wakati gari la polisi likiwasili eneo la tukio.
Polisi walimpiga risasi mtu huyo wakifikiri kufanya hivyo kutamaliza shambulio hilo, lakini aliendea kumng'ata mtuhumiwa wake jambo lililowashawishi kuendelea kumpiga risasi karibu mara 12 mpaka alipokufa.
Mwanaume huyo alifariki dunia mara alipofikishwa kwenye hospitali ya jirani kufuatia majeraha makubwa aliyopata kutokana na shambulio hilo.
Si mwanaume aliyekuwa uchi au mtuhumiwa wake aliyeweza kutambuliwa.
Mwanamke mmoja alimtaarifu polisi aliyekuwa karibu kwamba ameona wanaume wawili wakipigana, vyanzo vya habari zimesema.
Mfululizo wa milio ya risasi ilisikika eneo la MacArthur Causeway kando ya Mtaa wa North 13th.
Polisi alipowakuta wanaume hao, mwanaume aliyekuwa uchi alikuwa katika harakati za kumtafuna mwenzake usoni, ambaye pia hakuvaa nguo yoyote, imeripotiwa.
Ofisa wa Polisi alimtaka mwanaume aliyekuwa uchi kuacha alichokuwa akifanya.
Lakini alipokaidi kusikiliza na kuendelea kumtafuna mwenzake, ofisa huyo akamfyatulia risasi, kwa mujibu wa vyanzo vya habari.
Licha ya kupata jeraha la risasi, mwanaume huyo hakuacha hivyo polisi akalazimika kumpiga risasi zaidi ya sita.
Kwa mashambulizi hayo ya risasi, mwanaume aliyekuwa uchi akawa amekufa, akiwa ameelekeza kichwa chake ardhini.kwenye njia ya watembea kwa miguu jirani kabisa na maegesho ya magari ya Ofisiza gazeti la The Herald.
Msemaji wa Polisi, Javier Ortiz alisema kwamba kwa mujibu wa taarifa alizopokea, polisi aliyefyatua risasi 'ni shujaa na ameokoa maisha'.
Mtuhumiwa alisafirishwa kwenda Hospitali ya Jackson Memorial Ryder Trauma Center na kusema amekuwa akiugulia majeraha makubwa.
Wachache sana wanafahamu sababu zilizopelekea shambulio hilo, lakini polisi wanahisi kuwa mwanaume huyo aliyekuwa uchi hakuwa na sehemu ya kuishi.
Shahidi Larry Vega alisema: "Nilimsimamisha polisi wa Jiji la Miami na kumtaarifu kwamba mtu mmoja wa mitaani anamuua mtu kwa kumng'ata na kumrarua usoni."
"Polisi alimkabili mtu huyo na kama mbwa kichaa jamaa huyo akamgeukia polisi. Hapo polisi akampiga risasi mara nne," aliongeza.
Hakuna silaha yoyote iliyokutwa jirani na watu hao wawili, ikiongeza imani kuwa mshambuliaji alitumia nguvu yake binafsi kumdhuru mtuhumiwa wake.