CHEKA TARATIBU...
http://roztoday.blogspot.com/2012/08/cheka-taratibu_27.html
Afande kaenda kwenye nyumba ya mmiliki wa mbwa mmoja kushughulikia malalamiko dhidi ya mbwa wake. Mahojiano yakawa hivi:
Afande: Sahamani, mbwa wako amemkimbiza mtu kwenye baiskeli yake.
Mmiliki kwa ukali akajibu, "We kichaa nini? Mbwa wangu hajui kabisa kuendesha baiskeli!"
Afande akabaki mdomo wazi.
Posted by
Ekisha Admin