POLISI WAMCHUNGUZA MTALII ALIYEMCHOMA VISU MKEWE KWENYE BOTI...

Mtalii ambaye anadhaniwa kumchoma visu mpenzi wake safarini kwenye boti ya Uingereza anawezekana kuwa ni raia wa Marekani, polisi wamebainisha jana.
Wapelelezi wanaochunguza vifo kwenye eneo pana la Norfolk walisema watalazimika kusubiri kwa kitambo kirefu kabla ya kumtaja mtu huyo sababu mpangilio wake wa meno na rekodi nyingine zinahitajika kupatikana kutoka nje ya nchi.
Miili ya wapenzi hao, ambao wote wanakadiriwa kuwa na miaka 40 na kuishi maili 100 kutoka Surrey, ilikutwa ndani ya maji karibu na boti Jumapili iliyopita.
Binti wa mwanamke huyo mwenye miaka 13 alikutwa peke yake ndani ya chombo hicho, kilichokuwa kimefungwa sehemu ya faragha kwenye Mto Bure, karibu na Wroxham.
Wapelelezi wanachunguza uwezekano kwamba wapenzi hao walikufa kwa nyakati tofauti na kwamba mwanaume alimuua mwanamke kabla ya kujiua siku chache baadaye.
Sababu za awali ni kwamba mwanaume huyo amekufa kutokana na kuzama kwenye maji. Inadhaniwa alitumia pia njia nyingine, kama kujizidishia dozi ya dawa.
Matokeo ya uchunguzi wa miili hiyo yameonesha mwanamke alikufa kabla hajaingia kwenye maji, inawezekana kwamba alinyongwa.
Polisi, ambao walikuta vitu kadhaa ikiwamo shuka lenye damu kwenye begi ndani ya boti hiyo, jana walisema kuwa msichana huyo alikuwa akitafutwa na familia yake huko Norfolk.
Wapelelezi wanafanyia kazi kujua ni kwa muda gani msichana huyo wa miaka 13 alikuwa pekee kwenye boti kabla ya kukutwa na miili ya mama yake na mpenzi wake ilipogundulika kwenye mto.
Ripoti kadhaa zinasema kuwa boti hiyo ilifungwa sehemu hiyo kwa zaidi ya wiki huku mapazia yake yakiwa yamefungwa na ishara chache za uhai ndani yake.
Lakini ripoti nyingine zinaonesha familia ilikuwa ikifurahia nyamachoma huku boti hiyo ikiwa safarini Ijumaa usiku.
Mkuu wa timu ya upelelezi ya Norfolk na Suffolk alikataa kusema chochote juu ya taarifa hizo kwamba mwanamke ambaye hakutajwa jina lake, alikuwa amekufa kwa siku kadhaa.
Lakini imefahamika kuwa msichana, ambaye alikuwa peke yake ndani ya boti iliyokodiwa na familia yake, alikuwa akitunzwa na kulishwa wiki nzima iliyopita. Haikudhaniwa kama alikuwa amefungiwa ndani ya boti hiyo.
Udaku mmoja ulieleza kwamba mwanaume aliacha ujumbe kwa msichana huyo wakati akitoka kwenye boti hiyo, akimtaka kubaki ndani ya boti hiyo.
Muuza barafu, ambaye amefanya kazi eneo hilo kwa miaka 23, alisema boti hiyo imekuwa kwenye eneo hilo kwa 'takribani siku saba au nane'.
Baada ya kuona hakuna kusogea kwa boti hiyo wakati akipita eneo hilo kati ya Salhouse Broad na Wroxham Broad, karibu na Hoveton, akashawishika kwamba aende kuangalia kama kuna usalama ndani.
Muuza barafu huyo mwenye miaka 49 alisema: "Nilikwenda mara chache kwenye mto kuitazama na mara zote mapazia na madiridha yake yalikuwa yamefungwa hata wakati wa mchana.
"Jumanne majira ya Saa 11:30 jioni nikaamua kwenda na kuona kama kila kitu kilikuwa sawa sababu nilishawishika kujua usalama wao hasa kwa kuzingatia kwamba walikuwa sehemu ileile kwa muda mrefu sana.
"Nilikuwa kama umbali wa futi nane kutoka pale na kupiga kelele. Mwanaume akatoka akiwa mwenye haraka, kutokea eneo la chooni hadi nje eneo la wazi.
"Akanipigia kelele kupitia dirishani, "Ondoka. Sihitaji chochote", huku akinipungia mikono kuashiria kunifukuza. Nikaendelea kuiona boti ile mahali pale kila siku baada ya hapo."
Mmiliki wa Kampuni ya Fineway Launch Hire, Steve Daniels alisema kuwa wapitanjia wengi wamekuwa akiiona boti hiyo lakini hakufikiria kama kilikuwa si kitu cha kawaida.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item