HIVI NDIVYO SOKA ILIPOGEUKA KUWA BASKETBALL...
http://roztoday.blogspot.com/2012/10/hivi-ndivyo-soka-ilipogeuka-kuwa.html
Yaliwekwa kimiani jumla ya mabao 12 katika mchezo mmoja. Hii ilikuwa jana ambapo baada ya kukandamizwa 4-0, Arsenal iliweza kubadili matokeo na mwisho wa mchezo kuibuka na ushindi wa mabao 7-5 dhidi ya Reading katika mechi ya Kombe la Capital One na kufuzu kwa hatua ya Robo Fainali. Mabao ya Arsenal yaliwekwa kimiani na Theo Walcott aliyefunga mabao matatu kwa namna ya kipekee (Dakika ya 45, 90 na 120) huku mengine yakifungwa na Giroud, Kocielyn na Marouane Chamakh aliyefunga mawili. Hakika ilikuwa mechi ya ajabu!!