MAKARDINALI WAANZA LEO KUMCHAGUA PAPA MPYA...

Makardinali 115 wa Kanisa Katoliki wanaanza kumchagua Baba Mtakatifu Vatican leo.
Habari zilizotangazwa kutoka Vatican mwishoni mwa wiki, zinaonesha kwamba makardinali wote wamekufanyika katika makao makuu ya kanisa hilo tayari kwa kuanza kufanya uchaguzi wa kumchagua kiongozi wa ngazii ya juu katika kanisa hilo.
Uchaguzi huo unafanyika kutokana na Baba Mtakatifu Benedict wa 16 kujiuzulu Februari 28 mwaka huu baada ya kulitumikia kanisa kwa miaka minane na kitendo cha kujiuzulu kwake kilifanyika kwa mara ya mwisho takribani miaka 600 iliyopita.
Uchaguzi wa kiongozi huyo unafanyika baada ya Baba Mtakatifu kustaafu kutokana na umri wake wa  miaka 85 kuwa mkubwa lakini pia kutokana na afya yake kuzorota hivyo kutomudu kuendelea kuliongoza kanisa hilo.
Katika uchaguzi huo unaofanyika kwa siri (conclave), makardinali wenye haki ya kupiga kura ambao umri wao ni chini ya miaka 80 tangu kiti kilipokuwa wazi watapiga kura kwa siri mara tatu au nne kwa siku.
Upigaji kura utaendelea kufanyika kwa siri hadi mmoja wao atakapoibuka kuwa mshindi baada ya kupata kura theluthi mbili kura pamoja na kura yake mwenyewe ambayo huongezwa baada ya kuulizwa na kukubali kuchaguliwa huko, tendo la kukataa kuchaguliwa halijawahi kutokea tangu kanisa linaanza.
Katika uchaguzi huo, hakuna kardinali anayesimama kuwania nafasi hiyo, wote wanakuwa na nafasi sawa, lakini pia inawezekana kuchaguliwa askofu hata padri kushika wadhifa huo.
Uchaguzi huo utatanguliwa na misa maalumu ya kuombea uchaguzi huo leo asubuhi na ratiba inaonesha kwamba kura za kwanza zitaanza kupigwa mchana.
Wafanyakazi wa Vatican wameanza kuandaa ukumbi wa Sistine, ambapo mkutano wa uchaguzi utafanyika na kuandaa stovu mbili zitakazotumika kuchoma kura zilizopigwa.
Taarifa hiyo inasema, kura hizo zitachangwanywa zitatoa moshi mweusi na zitachanganywa na kemikiali ili kutoa moshi mweupe kama Baba Mtakatifu atakuwa amepatikana.
Uchaguzi wa Baba Mtakatifu katika mwaka 2005, uliwachukua makardinali siku tatu kumpata kiongozi huyo, jambo ambalo haijulikani watachukua siku ngapi kumpata kiongozi huyo na vyombo vingine vimetangaza kabla ya Machi 15 atakuwa amepatikana.
Makardinali 115 wanaoshiriki katika uchaguzi huo, 28 wanatoka nchini Italia na wengine kwenye mabano Marekani (11), Ujerumani (6), Brazili, India, Hispania (5), Ufaransa, Poland Magharibi (4), Canada, Poland Mashariki (3), Argentina, Nigeria, Ureno (2).
Kardinali mmoja anatoka Australia, Austria, Ubelgiji, Bolivia, Bosnia na Herzegovina, Chile, China, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Colombia, Croatia, Cuba , Jamhuri ya Czech, Jamhuri ya Dominican, Ecuador, Misri, Ghana na Guinea.
Wengine wanatoka nchi za Honduras, Hungary, Ireland, Kenya, Lebanon, Lithuania, Uholanzi, Peru, Philippines, Senegal, Slovenia, Afrika Kusini, Sri Lanka, Sudan, Uswisi, Tanzania,Uingereza, Venezuela na Vietnam.
Baba Mtakatifu atakaye chaguliwa atakuwa wa 266 tangu Mtakatifu Petro lakini atakabiliwa na changamoto nyingi zikiwamo za uzazi wa mpango, mapenzi ya jinsia moja na wanawake kuwa mapadri.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item