MKUU WA ITIFAKI WIZARA YA MAMBO YA NJE AVULIWA MADARAKA...

Balozi Anthony Itatiro.
Aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Itifaki, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Anthony Itatiro, amevuliwa madaraka yake.
Taarifa ya Serikali iliyotolewa jana jioni, imeeleza kuwa uamuzi huo wa kumvua madaraka Itatiro kwa kuhusishwa na jaribio la wizi wa Sh bilioni 3.5, ulishafanywa na Katibu Mkuu Kiongozi.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baada ya Itatiro kuvuliwa Ubalozi na Ukurugenzi, Katibu Mkuu Kiongozi ameamua apangiwe kazi nyingine kwa cheo cha chini ya alichokuwa nacho.
Katika hatua nyingine, taarifa hiyo ya Serikali ilieleza kuwa hakuna wizi wowote ulitokea Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kama ambavyo imeandikwa na kukaririwa na baadhi ya vyombo vya habari.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa uchunguzi uliofanywa na timu maalumu iliyohusisha vyombo mbalimbali vya kifedha, ulinzi na usalama, ilibaini kwamba hakuna wizi uliotokea isipokuwa kulikuwa na uzembe katika kusimamia utaratibu.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item