MPAGAZI ALIYEMBAKA NYOTA WA RUNINGA HOTELINI AFUNGWA MIAKA 10 JELA...

KUSHOTO: Mahakama ambako hukumu hiyo ilitolewa. KULIA: Soby John.
Nyota wa runinga alibakwa kwenye chumba chake hotelini na mpagazi wa Kihindi ambaye alikuwa akisubiria kurejeshwa kwao, mahakama ilielezwa juzi.

Soby John, mwenye miaka 25, alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela baada ya kukiri kuvamia chumbani mwa muathirika huyo katika hoteli moja maarufu mjini London na kumfanyia unyama huo wakati akiwa amelala, katika kile jaji huyo alichoeleza kama shambulio la 'udhaifu'.
Nyota huyo alikuwa amekunywa mno pombe katika klabu ya West End akiwa na marafiki zake jioni ya siku hiyo na 'hakuwa na uwezo wa kujitetea mwenyewe'.
John, ambaye alikuwa akiishi Wembley, aliingia nchini Uingereza kwa kutumia viza ya masomo lakini ilikwisha muda wake na alikuwa akisubiri kurejeshwa nchini India.
Alikuwa amezawadiwa kazi ya zamu katika hoteli hiyo kupitia wakala katika usiku huo wa shambulio hilo mwaka jana
Mahakama ilielezwa alitumia nafasi yake kama mpagazi kupata nakala ya ufunguo wa elektoniki kwenye chumba cha muathirika huyo baada ya kumuona akipepesuka katika kibaraza cha hoteli na kusaidiwa kwenda kulala na rafiki yake wa kike katika saa za mapema za Oktoba 24.
Mwendesha mashitaka Lesley Jones, alisema John aliingia kwenye chumba cha muathirika kwa kutumia funguo hizo na kumbaka wakati akiwa amelala kitandani.
Alisema: "(Muathirika) aliamka usiku huo na kumwona mwanaume wa Kiasia akiwa juu yake akiwa anafanya naye mapenzi."
Muathirika huyo 'alijihisi kutokuwa na nguvu na kushindwa kujitetea mwenyewe', alisema, na kuongeza: "Alisema alihisi mkono wa mwanaume huyo shingoni mwake wakati akimsukumizia mbali lakini  baadaye akapoteza fahamu."
Baada ya kumbaka, John alipiga picha kwenye simu ya nyota huyo ya iPhone na kujitumia picha hizo kwenye simu yake.
Katika jaribio la kufanya ubakaji huo kuonekana wa makubaliano, pia alituma meseji kutoka kwenye simu ya nyota huyo kwenda kwake, ikisema: "Hey John umenifurahia nashukuru'.
Alama zilizochukuliwa kutoka kwa muathirika huyo zilioana na vipimo vya DNA vya John, kama ilivyokuwa DNA iliyochukuliwa kutoka kwenye glovu mbili zilizotelekezwa kwenye chumba hicho ambacho mahakama ilielezwa kilitumika kama kondomu 'ghafi'. John alikiri kufanya mapenzi na mwanamke huyo pale polisi walipotumia taarifa kutoka kwa walinzi wa hoteli kumfuatilia hadi nyumbani, lakini alikana kubaka katika mahojiano ya awali.
Alibadili ombi lake la hatia mnamo Februari.
Juzi kwenye Mahakama ya Southwark, wakili wa utetezi Peter Higginson alisema mteja wake alikuwa 'kijana mshamba, akihangaika katika utamaduni ambao hakuwahi kuweza kuendana nao'.
Alisema John hakuwahi kutiwa hatiani nchini Uingereza au India, kwamba mara zote alifanya kazi na 'hakuwahi kujisumbua' katiki hali hiyo.
Mahakama hiyo ilielezwa kwamba John atarejeshwa kwao India mara tu atakapomaliza adhabu yake.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item