AGONGWA NA NYOKA KWENYE UUME WAKATI AKIJISAIDIA CHOONI...

Aina ya nyoka wa jamii hiyo.
Mwanaume mmoja amekimbizwa katika hospitali moja baada ya nyoka kumng'ata kwenye uume wake wakati akijisaidia chooni, kwa mujibu wa maofisa wa hospitali nchini Israeli.

Mtu huyo, mwenye miaka 35, kutoka kaskazini mwa Israeli aling'atwa Ijumaa baada ya nyoka huyo ghafla kuchomoza kutoka ndani ya choo hicho.
Mwanaume huyo alipata majeraha madogo kutokana na kung'atwa huko; kwa bahati nzuri nyoka huyo hakuwa mwenye sumu.
Waokoaji walifika eneo la tukio na kumchukua mtu huyo hadi Kituo cha Afya cha Rambam mjini Haifa, ambako alipatiwa matibabu, limeripoti Your Jewish News.
Uchunguzi ulibainisha nyoka huyo hakuwa mwenye sumu.
Mwanaume huyo aliwaeleza wafanyakazi wa dharura ilitokea baada ya kwenda chooni kujisaidia na ghafla akahisi maumivu makali ya kuungua katika uume wake.
Mmoja wa wahudumu alisema mwanaume huyo alimweleza alikuwa amemwona nyoka huyo na kwamba alikuwa mdogo mno.
Kwa mujibu wa madaktari, licha ya eneo la jeraha, mwanaume huyo alifanikiwa kubaki kimya na hata kutaniana na wafanyakazi kwa gharama yake.
"Hii ni mara ya kwanza kuona nyoka aking'ata kama hivi," walisema wafanyakazi hao.
"Kwa bahati, vipimo vyote vinaonesha viko safi na mtu huyo anaendelea vizuri," waliongeza wafanyakazi hao.
"Alama za kung'atwa zilionekana dhahiri kwenye eneo la uume," ilisema hospitali hiyo.
"Nyoka huyo hakuwa na sumu. Mtu huyo kwa sasa yuko chini ya uangalizi maalumu akisubiria majibu zaidi ya vipimo na mara tu yatakapopatikana, ataruhusiwa kwenda nyumbani," ilisema hospitali hiyo.
Mwanaume huyo alikuwa na bahati kwamba nyoka huyo hakuwa mwenye sumu kutokana na kuwapo nyoka wengi wenye sumu kali wanaopatikana zaidi nchini Israeli.
Nyoka wana tabia ya kujilinda mno na hushambulia kulinda himaya yao, iwe kwenye mwamba au vyoo vya nyumbani.
Ni 'msimu wa nyoka' kwa sasa katika Mashariki ya Kati na miongoni mwao hatari zaidi ni nyoka weusi au cobra wa jangwani, Kipiribao wa Palestina ambao ni maarufu sana wenye sumu kali nchini Israeli.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item