CHADEMA YATETEA KATA NNE UCHAGUZI MDOGO UDIWANI ARUSHA...
http://roztoday.blogspot.com/2013/07/chadema-yatetea-kata-nne-uchaguzi-mdogo.html
Zoezi la kuhakiki kura likiendelea katika Kata ya Kaloleni. |
Matokeo ya awali ya uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata nne mkoani Arusha, yameonesha kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeongoza katika kata zote nne za udiwani Arusha.
Katika matokeo hayo, Chadema imeonekana kuongoza karibu katika kila kituo cha uchaguzi, huku ikifuatiwa na CCM. Baadhi ya vyama vingine vimepata kura chache na vingine kukosa kabisa.
Katika Kata ya Kaloleni kituo A 1: CCM 17, Chadema 37 na CUF 3 Kituo A2 Chadema 28, CCM 16, CUF 2 na Kituo A3: CCM 13, Chadema 28 na CUF 2.
Katika Kata ya Elerai, Kituo cha Sekondari: CCM 18, Chadema 39, CUF 3 na A2: CCM 12, Chadema 21 na CUF 6. D1 Chadema 42, CCM 15 na B 2, Chadema 42, CCM 11. C 1 CCM 12, Chadema 35 na CUF 3, ambapo C 2 CCM 26, Chadema 28 na CUF 3. Shule ya Msingi Burka, CCM 31, Chadema 30 na CUF 2; E3 CCM 41, Chadema 43, CUF 5. D4 Chadema 32, CCM 30 na CUF 5.
Katika kata za Themi na Kimandolu, taarifa zilizolifikia gazeti hili, zilionesha Chadema imeendeleza ushindi karibu katika vituo vyote na kufuatiwa na CCM.
Wagombea udiwani Kata ya Elerai na vyama vyao ni Mwalimu Emmanuel Laizer (CCM), Gilbert Bayo (CUF), Seif Shimba (CCK), Jeremiah Mpinga (Chadema) na Boisafi Shirima (TLP).
Kata ya Kaloleni ni Emmanuel Mliari (CCM), Darwesh Mkindi (CUF), Kessy Lewi (Chadema) na Ngilishi Pauli (Demokrasia Makini).
Katika Kata yaThemi ni Victor Mkolwe (CCM), Kinabo Edmund (Chadema), Lobora Ndaproi (CUF) na Kata ya Kimandolu ni Edna Saul (CCM) na Rayson Ngowi (CHADEMA).