MAMA AIJIA JUU SHULE KWA KUMNYIMA MWANAE MAJI SABABU YA MFUNGO...
http://roztoday.blogspot.com/2013/07/mama-aijia-juu-shule-kwa-kumnyima.html
KUSHOTO: Shule ya Msingi Charles Dickens. KULIA: Kora Blagden. |
Mama aliyejawa na hasira ameishutumu shule moja msingi kwa kumkatalia mwanae maji ya kunywa katika moja kati ya siku zenye joto kali katika mwaka kwa kuhofia kuwatibua wanafunzi waliofunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Kora Blagden, mwenye umri wa miaka 32, alidai mwalimu mmoja kwenye shule anayosoma mwanae Luke alikataa kumruhusu mtoto huyo mwenye miaka 10 kutoa chupa yake na kunywa maji sababu hakuwa akiwatendea haki wanafunzi wenzake waliofunga.
Wanafunzi wengi katika Shule ya Msingi Charles Dickens, huko Portsmouth, Hampshire, wanafunga wakati huu wa Ramadhani, ambayo inamaanisha wanazuiwa kula au kunywa maji kati ya alfajiri na jioni kwa takribani siku 30, kutegemea na kuonekana mwezi.
Mama wa watoto wanne, Kora alisema: "Muda mfupi kabla ya kulala mimi na watoto wangu wa kiume, Luke mwenye miaka 10, na Alfie, mwenye miaka minane, tulikuwa tukiongelea kuhusu Ramadhani kama tulivyokuwa tumeona kwenye taarifa za habari.
"Luke aliniambia alielezwa na mwalimu wake kwamba haruhusiwi kunywa maji darasani.
"Sababu iliyotolewa, mtoto mmoja anayefuna alikuwa akiumwa kichwa na mwalimu huyo alisema haitokuwa haki kama wanafunzi wengine wakinywa mbele ya wanafunzi hao.
"Kwa kawaida wanakuwa na chupa zao juu ya meza zao lakini zilikuwa zimewekwa kwenye trei na mwalimu huyo.
"Alikuwa nayo pembeni yake lakini alikuwa na kiu na hakutaka kuwakosea wanafunzi hao wengine.
"Alfie alisema aliruhusiwa kunywa wakati wa asubuhi lakini si mchana.
"Luke alikuwa ameishiwa maji mwilini pale alipofika nyumbani na kunywa glasi tatu za maji bila kupumzika."
Mwalimu huyo alitoa mari hiyo Alhamisi wakati joto lilipofikia hadi nyuzi 28.
Blagden alimkabili mwalimu mkuu msaidizi Lisa Florence kabla ya masomo kuanza jana na kuombwa radhi kwa mdomo kwa tukio hilo.
Alisema: "Niliongea na mwalimu mkuu msaidizi na kuwaeleza alichoniambia Luke na nikauliza kwanini hili liliruhusiwa kutokea.
"Alisema haikuwa haki kwa mwanangu kukataliwa kunywa maji katika kipindi na hivyo kubaki na kiu yake wakati wote siku nzima.
"Alisema watazungumza na Luke na mwalimu huyo, na kusema samahani kwa watoto wangu kushindwa kunywa maji.
"Mkuu huyo msaidizi alisema hicho sicho walichoambiwa kufanya na ni kile tu ambacho watoto wenye imani ya Kiislamu wanafanya.
"Sina tatizo na hilo lakini sitarajii wanangu kuambiwa hawawezi kunywa maji.
"Binafsi nafikiri ni makosa makubwa."
Charles Dickens ni shule iliyoko katikati ya jiji mitaa michache kutoka sehemu aliyozaliwa mwandishi maarufu duniani mwenye jina kama hilo.
Shule hiyo ilisema hakukuwa na kizuizi kwa watoto kutoka dini nyinginw kula chakula na vinywaji wakati wa mfungo wa Ramadhani lakini ilikataa kuzungumzia kuhusu suala hili binafsi.
Halmashauri ya Mji wa Portsmouth, ambayo linaendesha shule hiyo yenye watoto 300, pia ilikataa kuzungumzia suala hilo.