MAMA AMCHOMA MARA 90 USONI MTOTO WAKE WA MIEZI 8...KISA? KAMNG'ATA CHUCHU AKINYONYA...

Mtoto Xiao Bao akiwa amelazwa hospitalini baada ya kushambuliwa na mama yake mzazi.
Mtoto wa kiume mwenye umri wa miezi minane ana bahati kuwa hai baada ya kuwa amechomwa na kitu chenye ncha kali mara 90 na mama yake, hasa usoni, kwa kumng'ata chuchu wakati akimnyonyesha.

Xiao Bao alilazimika kushonwa zaidi ya nyuzi 100 baada ya tukio hilo mjini Xuzhou, mashariki mwa jimbo la Jiangsu nchini China.
Mtoto huyo mchanga anaishi na mama yake na wajomba zake wawili, ambao wanaishi kwa kutegemea kuzalisha taka. Alikuwa mmoja wa wajomba zake ambaye alimgundua Xiao Bao akiwa amelala kwenye dimbwi la damu katika eneo la nyumba yao na kumuwahisha hospitali.
Mama wa mtoto huyo baadaye alikiri kwamba alimchoma mtoto huyo baada ya kuwa amemng'ata kwenye chuchu yake wakati akimnyonyesha.
Majirani waliiomba serikali ya eneo hilo kumwondosha mtoto huyo mbali na mama yake, lakini wamesema hawatafanya hivyo.
Inavyoonekana, walisema kwamba hakukuwa na uthibitisho mama huyo alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya akili na kusema, bila kujali, mtoto huyo bado ana waangalizi wawili kwa maana ya  wajomba zake wawili.
Maradhi ya akili yamekuwa mada kuu katika China ya sasa, na si matibabu wala tiba ya kisasa ya akili inayotumika kwa mapana.
Uchunguzi wa masuala ya afya ya akili katika majimbo manne nchini China, uliochapishwa mwaka 2009 kwenye jarida la tiba la Uingereza la The Lancet, ulikadiria kwamba asilimia 91 ya watu wazima milioni 173 nchini China ambao wanaaminika kusumbuliwa na matatizo ya kiakili hawajawahi kupata msaada wa kitaalamu.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item