MSICHANA ABAKWA AKIPITA UFUKWENI ASUBUHI NA MAPEMA...
http://roztoday.blogspot.com/2012/09/msichana-abakwa-akipita-ufukweni.html
Ufukwe wa Brighton ambapo msichana huyo alibakwa na wanaume wawili huku mwingine akishuhudia pembeni.
Msichana mwenye miaka 19 amebakwa na wanaume wawili katika ufukwe wa Brighton huku mwanaume mwingine akishuhudia, polisi walisema jana.Msichana huyo, anayetokea Kent, aliwaeleza maofisa wa polisi alikokotwa na wanaume wawili wenye umri wa miaka inayokadiriwa kuwa 30 na kubakwa mapema asubuhi huku mtu wa tatu akiwa kasimama kando.
Shambulio hilo lilitokea ufukwe wa kati ya klabu ya usiku ya Coalition na Regency Square.
Msichana huyo alikuwa katika matembezi na rafiki yake mapema jioni lakini akaamua kurudi kwenye hoteli ambako alikuwa alikofikia.
Mpelelezi Sajenti Graham Lewendon kutoka Polisi Sussex alisema: "Hili lilikuwa tukio la kuhuzunisha kwa mwanamke na tunampatia msaada wetu.
"Tunaomba raia mwema yeyote ambaye anaweza kutusaidia kuwapata watuhumiwa.
"Tungependa kuongea na yeyote aliyemuona msichana huyu karibu na klabu ya usiku ya Coalition au yeyote aliyewaona wanaume watatu wenye mashaka au wakikimbia.
"Usiku wa leo tunaongeza maofisa wetu katika eneo hilo kuongea na watu na kuwashauri na kuwahakikishia usalama wao. Pia tutakuwa tukitafuta mashuhuda wowote wa tukio hilo.
"Uchunguzi uko katika hatua zake za awali na tunashughulika na muathirika kuweza kujua mazingiza ya tukio lenyewe."
