BASI LA METRO LAGONGANA USO KWA USO NA FUSO...

Lori hilo aina ya Fuso likiwa katika eneo la ajali.
Basi la Metro lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Arusha, limepata ajali katika eneo la Kawawa wilayani Moshi na kusababisha kifo cha dereva wa basi hilo, aliyefahamika kwa jina moja la Oscar.

Ajali hiyo ilitokea juzi saa moja usiku basi hilo,  lilipogongana uso kwa uso na lori aina ya Fuso, lililokuwa likienda Njia Panda katika Mji wa Himo na majeruhi sita walikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC.
Mashuhuda wa ajali hiyo, walisema dereva wa Fuso alikuwa akijaribu kupita lori jingine aina ya Scania, lenye tela kabla ya kukutana na basi la Metro na kugongana uso kwa uso.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo. Alisema magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni basi la Metro aina ya Yutong, lenye namba za usajili  T 129 BQL likiendeshwa na Oscar na Fuso lenye namba za usajili T 615 AWB, lililokuwa likiendeshwa na Goodluck Aseri (45).
Boaz alisema miongoni mwa majeruhi waliokimbizwa KCMC, yupo kondakta na abiria wengie watano katika basi hilo.
Alisema Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, inamshikilia Dereva wa Fuso kwa maelezo zaidi na mara baada ya uchunguzi atafikishwa mahakamani kwa mujibu wa Sheria ya Usalama Barabarani.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item