BINTI ALIYEBAKWA NA WALIMU WAKE WATATU AJIFUNGUA MTOTO ALIYEZAA NA BABU WA MIAKA 74...
http://roztoday.blogspot.com/2013/07/binti-aliyebakwa-na-walimu-wake-watatu.html
Binti huyo akiwa amempakata mtoto wake wa kike. |
Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 12 amejifungua mtoto ambaye alidaiwa kuzaa na babu mwenye miaka 74.
Mstaafu huyo kutoka kijiji cha jirani huko Qiyang, jimbo la Hunan, nchini China amekamatwa na polisi kwa uhalifu huo baada ya ushahidi wa kipimo cha DNA kuripotiwa kufichua kwamba alikuwa baba wa mtoto huyo wa kike.
Lakini msichana huyo amekanusha kwamba alibakwa na mzee huyo.
Badala yake anadai kwamba alikuwa amebakwa kwa kujirudia-rudia na walimu wake watatu.
Familia yake inaamini kwamba mstaafu huyo alikuwa amelazimishwa kukiri kama sehemu ya kuwaficha ukweli polisi.
Wanaamini kwamba DNA haikuwa imechukuliwa kutoka kwa yeyote kati ya walimu hao watatu kuona kama walikuwa baba wa binti yake huyo.
Msichana huyo pia anadai kwamba wakati fulani uchunguzi ukiendelea aliwaona walimu hao watatu katika namna iliyomwacha na maswali wakimkabidhi fedha polisi.
Anadai pia alipewa vitisho na mwalimu mkuu wa shule yake ili akae kimya.
Babu huyo amehukumiwa kifungo cha miaka 12 jela.