WATUMISHI WA NDANI SASA KULIPWA SHILINGI 35,000 KWA WIKI...
http://roztoday.blogspot.com/2013/07/watumishi-wa-ndani-sasa-kulipwa.html
Mshahara wa watumishi wa ndani, sasa umewekwa kisheria kuanzia Julai mosi, kupitia tangazo la Serikali la Kima cha Chini cha Mshahara wa Kisekta, lililotolewa na Msemaji wa Wizara ya Kazi na Ajira, Ridhiwani Wema.
Kwa mujibu wa tangazo hilo lililochapishwa jana katika vyombo vya habari, wafanyakazi wote wa ndani walioajiriwa, mbali na wanaofanya kazi za ndani kwa makubaliano mengine yasiyo ya ajira, kama muda mfupi na kuacha, wanapaswa kulipwa si chini ya kiwango kilichotajwa kisheria.
Watumishi hao wamepangwa kwa madaraja, ambapo daraja la kwanza litahusu watumishi wa ndani katika nyumba za waajiri wenye hadhi ya kibalozi na wa mashirika ya kimataifa.
Daraja hilo la kwanza litahusu pia watumishi wa ndani katika nyumba za wafanyabiashara mashuhuri, ambao kwa pamoja watalipwa kwa mwezi si chini ya Sh 150,000, ambayo ni sawa na Sh 34,618 kwa wiki, Sh 5,769.70 kwa siku na Sh 769.30 kwa saa.
Watumishi katika nyumba za maofisa wenye nafasi za juu, watakuwa daraja la pili na kulipwa si chini ya Sh 130,000 kwa mwezi, sawa na Sh 30,002.30 kwa wiki, Sh 5,000.40 kwa siku au Sh 666.70 kwa saa.
Katika daraja la tatu, kima cha chini kinahusu watumishi wa ndani ambao wanafanyakazi kwa watu wengine mbali na maofisa wenye hadhi ya kibalozi, wafanyabiashara mashuhuri na maofisa wa juu.
Watumishi hao ni wanaofanya kazi na kuondoka jioni, ambao mshahara wao wa kima cha chini kwa mwezi utakuwa si chini ya Sh 80,000, sawa na Sh 18,463 kwa wiki na Sh 3,077.15 kwa siku au Sh 410 kwa saa.
Daraja la mwisho ni kwa wafanyakazi wengine wa ndani, ambao mshahara wao wa kima cha chini, utakuwa si chini ya Sh 40,000.
Watumishi hao mapato yao hayajatafsiriwa kwa wiki, siku au saa lakini ndio wanaolipwa kima kidogo kuliko sekta zingine nchini.
Sekta zilizoongoza kwa kuwa na kima cha chini cha mshahara, ambacho ni kikubwa kwa mwezi, ni sekta ya mawasiliano ya simu, huduma za kifedha, migodi iliyothibitika kuwa na madini, na kampuni za kimataifa za nishati ambazo kima cha chini ni Sh 400,000 kwa mwezi.
Sekta zinazofuata kwa kuwa na kima cha chini chenye mshahara mnono kwa mwezi ni sekta ya ujenzi kwa kampuni za ujenzi za daraja la kwanza, ambayo kima cha chini ni Sh 325,000.
Kwa mujibu wa sheria hiyo, wafanyakazi katika usafiri wa anga, kampuni za upakiaji na upakuaji mizigo na kampuni zinazotafuta madini, kima cha chini kinapaswa kuwa Sh 300,000.
Watumishi katika kampuni za ujenzi daraja la pili mpaka la nne, watalipwa si chini ya Sh 280,000, wakifuatiwa na watumishi wa kampuni za ujenzi daraja la tano mpaka la saba na wa hoteli za kitalii ambao kwa mwezi kima cha chini kimetajwa kuwa Sh 250,000.
Kwa wafanyakazi wa kampuni za usafirishaji za majini na nchi kavu, wakiwemo madereva na makondakta wa daladala na kampuni za uvuvi, kima cha chini kitakuwa Sh 200,000.
Wafanyakazi katika kampuni za habari, posta na usafirishaji wa vifurushi na kampuni za kimataifa za ulinzi, kampuni ndogo za kuzalisha nishati na hoteli za kati, kima cha chini kitakuwa Sh 150,000, kikifuatiwa kwa karibu na kima cha chini kwa shule binafsi za sekondari mpaka chekechea, ambacho ni Sh 140,000.
Katika sekta ya afya, kima cha chini kitakuwa Sh 132,000, kikifuatiwa na hoteli, nyumba za kulala wageni na baa Sh 130,000, biashara na viwanda, sekta ya kilimo na zingine ambazo hazijatajwa itakuwa Sh 100,000.
“Kima cha chini kama kilivyoainishwa, kitatafsiriwa kama kiwango cha chini cha mapato atakayopewa mwajiriwa katika sekta husika. Mwajiri anaweza kumlipa mwajiriwa mapato ya juu zaidi, lakini hapaswi kulipa chini ya mapato yaliyowekwa na sheria.
“Mwajiriwa pia anastahili kupata likizo ya malipo kila mwaka na posho ya usafiri mara moja kila baada ya miaka miwili ya kufanya kazi kwa mwajiri mmoja,” ilifafanua sheria hiyo.
Sheria hiyo pia inamtaka mwajiri ambaye anamlipa mtumishi wake vizuri kuliko kima cha chini kilichotangazwa, aendelee kumlipa mapato hayo na mafao mengine anayostahili.
Pamoja na tangazo hilo, tayari kumekuwa na malalamiko ya baadhi ya kada ya watumishi kulipwa kiasi kidogo cha mishahara na hivyo kuwafanya washawishike kuiba na wengine kujiuza.
Kada ya watumishi wa baa na nyumba za kulala wageni na huduma zifananazo na hizo, wamekuwa waathirika wa malipo hayo ya chini na hata kupunjwa au kudhulumiwa na waajiri wao.