CHEKA TARATIBU...

Mchungaji mmoja wa Kanisa moja Arusha yuko hoi kitandani akikaribia kukata roho. Ndipo akatuma ujumbe kuwaita Mhasibu na Mwanasheria wake, na baadhi ya waumini wa kanisa hilo.
Wote wakaitikia wito na kufika hadi nyumbani kwa Mchungaji na moja kwa moja wakaelekea kitandani na kumzunguka wakisikiliza anachotaka kuwaeleza.
Mchungaji akawashika mikono Mhasibu na Mwanasheria kisha akatazama juu bila kusema neno na kutabasamu. Baada ya hapo akaagiza wale waumini wengine wote waondoke wakaendelee na majukumu yao mengine.
Huku akiwa kawashika mikono mmoja upande huu wa kitanda na mwingine upande ule, akaendelea kubaki kimya huku akiwa kafumba macho bila kuongea chochote kwa zaidi ya saa nzima. Ndipo Mhasibu akavunja ukimya na kuuliza, "Mchungaji kama huongei kitu, sasa kwanini ulituita hapa?"
Kwa taabu na maumivu makali, Mchungaji akajibu kwa sauti ya kigonjwa, "Yesu alikufa katikati ya wezi wawili, na hivi ndivyo nataka itokee." Alaa kumbe...

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item