MWALIMU ALIYEKAA UCHI MBELE YA WANAFUNZI ATIWA HATIANI...
https://roztoday.blogspot.com/2013/01/mwalimu-aliyekaa-uchi-mbele-ya.html
David Braidley akiwa nje ya lango kuu la kuingilia shuleni kwake. |
Mwalimu ambaye alitunukiwa heshima ya MBE na Malkia amepatikana na hatia ya kukiuka maadili ya kazi yake baada ya kukaa uchi na wanafunzi wakati wa safari yao nje ya mipaka ya shule.
David Braidley mwenye miaka 55, pia alivua nguo kwenye eneo la bafu ambako watoto, wenye umri wa miaka 12 na 13, walikuwa wako uchi.
Na katika tukio jingine alimkumbatia mwanafunzi wa kike.
Pia aliongoza shindano lisilo la kawaida la 'kukojoa' kati ya wanafunzi kutoka Shule ya Sarufi ya North Cestrian, Altrincham, Cheshire, katika safari ya kambi hiyo hiyo kati ya Novemba 4 na 6, 2011.
Tukio hilo lilitokea wakati akiwa kiongozi wa wanafunzi 11 ambao walikuwa wakikaa katika kituo cha Solwaybank mjini Dumfries na Galloway, nchini Scotland.
Braidley alitunukiwa heshima ya MBE mwaka 2008 kwa huduma yake kwa vijana baada ya kuongoza tuzo ya mpango wa Mwana Mfalme wa Edinburg kwa miaka 30.
Juzi mwanandoa Braidley, kutoka Hale Barns, Greater Manchester, alipatikana na hatia ya kujihusisha na taaluma isiyokubalika katika kikao cha nidhamu cha Wakala wa Ualimu mjini Coventry.
Jopo hilo liligundua ilikuwa haifai kwa yeye kukatiza akiwa uchi kwenye eneo ambalo limejaa wanafunzi.
Alikiri alivua nguo mbele ya wanafunzi wa kiume wakati wakioga na kukaa kumpakata mapajani mwanafunzi wa kiume, lakini hili halikutosha kumweka katika kiwango cha kukiuka maadili.
Braidley pia alikiri kuwakumbatia wanafunzi wa kike lakini alifutia hatia ya kukiuka maadili pale alipodai alimshika sababu alikuwa na mashaka kuwa anaumwa.
Pia alikiri kuwauliza wavulana wawili kama wangefanya 'mashindano ya kukojoa' kabla ya kusema 'kaa tayari twende' lakini hili pia liliamriwa haikuwa tabia isiyofaa.
Madai kwamba alishauri kuwapa wanafunzi faini kwa kuwakalisha kwenye glasi ya baridi hayakuweza kuthibitishwa.
Kuamua kukatiza uchi haikufikia kiwando cha ukiukaji maadili, mwenyekiti wa jopo hilo John Pemberton alimweleza: "Walimu wana jukumu kubeba imani ya jamii kwenye taaluma yao na kuendeleza viwango vya juu vya tabia ndani na nje ya shule.
"Katika tukio hili umeshindwa kudhibiti mipaka inayofaa na kuonesha kinaganaga tabia inayofaa kuwepo kati ya wanafunzi na walimu.
"Tumeridhishwa kwamba vitendo vyako vinafikia kiwango cha ukiukwaji wa taaluma yako ambavyo vinafanya taaluma isiheshimike."
Katika kikao hicho cha siku moja, Braidley alidai alisukumwa na wanafunzi kadhaa wa kiume kukatiza uchi wakati kundi hilo lilipopiga kambi katika ghala la nafaka.
Alilieleza jopo: "Vijana walishavua nguo kwa masihara na walikuwa wakisema "njoo mheshimiwa, ni zamu yako sasa."
"Wakati fulani, bila kujijua nikaenda, nikakimbia kuelekea chini bustanini na kurudi pale.
"Hata wakati nikifanya nilijiuliza 'nafanya nini hiki?"
"Wakati huo na pia muda mfupi baadaye nikagundua haikufaa kufanya vile.
"Niliwaza 'upuuzi gani huu unafanya? Sijawahi kufanya hivi hapo kabla kwanini nafanya sasa?"
Braidley, ambaye anafundisha Kiingereza kwa miaka 37, pia alikiri 'hakuwa sawa' na kusema alikuwa 'kapigwa na butwaa' kwamba utamaduni wa njia za ufundishaji zilikuwa sasa zikichukuliwa 'zinatia hofu.'
Alisema: "Kitu kilichonijia katika hili ni jinsi ambavyo sikuwa sawa.
Akizungumzia kuhusu tukio ambapo alimkumbatia mwanafunzi wa kike na kumpakata mwanafunzi wa kiume, Braidley alisema alikuwa akijaribu kupata joto la mwili na kuwafanya wapate joto.
"Alisema: "Wote walichukulia kama vitu vinavyotakiwa kufanywa.
"Naamini nilichofanya pale kilikuwa kinachotakiwa kufanywa na mawalimu anayejali, mzazi anayejali, na kile ambacho mwanadamu angefanya.
"Kumtelekeza mtoto akiumwa ni kukosa utu."
Bradley hajafanya kazi shuleni hapo tangu madai hayo yalipowasilishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2011.
Msemaji wa shule alisema alikuwa amesimamishwa kupisha uchunguzi wa ndani, wakati akisubiria kustaafishwa kwake mapema kwa lazima.
"Mwalimu anayehusika alisimamishwa mara moja kupisha uchunguzi wetu wenyewe wa ndani.
"Hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na Mamlaka za Kisheria dhidi ya Bradley.