MWALIMU WA KIKE ABAMBWA AKIFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI WAKE NDANI YA GARI...

KUSHOTO: Chuo alichofundishwa mwalimu huyo. KULIA: Mwalimu Eppie Sprung Dawson.
Mwalimu aliyeaibishwa ambaye alikamatwa ndani ya gari akiwa na mwanafunzi mwenye miaka 17 juzi alikiri kwamba alikuwa akifanya mapenzi na kijana huyo.

Mahakama ilielezwa jinsi Eppie Sprung Dawson, mwenye miaka 26, alivyomkubalia kijana huyo asiyeweza kusoma vizuri msaada wa ziada katika masomo yake kwenye shule ya sekondari ya Katoliki ambako alikuwa akifanya kazi.
Lakini mwalimu huyo Mwingereza aliyeolewa, ambaye alikuwa na miaka minne tu kwenye kazi yake hiyo, alimpeleka mtoto huyo nje ya mji, akasimamisha gari kando na kufanya naye mapenzi.
Walikutwa wakiwa pamoja na maofisa wa polisi waliokuwa katika doria ya kawaida.
Katika Mahakama ya Dumfries Sheriff juzi, Dawson alikiri kwamba Desemba 21, akiwa kwenye dhamana ya uaminifu, alijiingiza katika vitendo vya kimapenzi na, au kuelekeza, mtu aliye na umri chini ya miaka 18, na kwamba alihusiana naye kimapenzi.
Mwendesha mashitaka Lyndsay Hunter alisema kwamba Dawson alikutana na kijana huyo mjini Dumfries na kisha kumchukua kwenye gari lake hadi Barabara ya Hoddam.
Alisema kwamba mnamo majira ya Saa 11:20 jioni, polisi walibaini gari hilo, ambalo lilikuwa na ukungu kwenye madirisha yake.
Hunter aliongeza: "Maofisa hao walibaki kwenye gari lao na kushuhudia wawili hao wakiwa kwenye kiti cha abiria cha gari hilo.
"Waliliacha gari lao na kuelekea kwenye gari hilo lililoegeshwa ambako waliwaona wapenzi hao wakiwa wanafanya mapenzi.
"Maofisa hao wa polisi waligonga mlango wa gari hilo na kisha wakamwona mtuhumiwa na mwanaume, wote wakiwa bila nguo kutoka juu hadi chini."
Hunter alisema kwamba Dawson aliongea nao na ikafahamika bayana kwamba alikuwa mwalimu.
Mwendesha mashitaka huyo aliongeza kwamba Dawson hakujibu wakati alipoonywa na kushitakiwa.
Hukumu imeahirishwa hadi Mei Mosi, ripoti itakapowasilishwa na uchunguzi wa daktari utakapokamilika.
Dawson, mkazi wa Dumfries, ambaye alisoma kwenye chuo cha St Joseph, ameorodheshwa kwenye orodha ya washitakiwa wa udhalilishaji.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item