MWANAMKE AFANYA MAPENZI NA WATOTO WAWILI HUKU WENZAO WAKISHUHUDIA...

KUSHOTO: Tom Shimandale. KULIA: Jeanine Shimandale.
Mwanamke wa Florida aliyeolewa mwenye miaka 42 amekamatwa baada ya polisi kusema alifanya mapenzi na watoto wadogo wawili, mmoja kati yao akiwa mdogo wa miaka 13, huku watoto wengine wakishuhudia.

Ofisi ya Mkuu wa Usalama wa Jimbo la Sarasota ilisema kwamba Jeanine Shimandale, wa Bradenton, sasa anakabiliwa na mashitaka manne ya uasherati na ukware na mashitaka mawili ya kuchangia kwenye uhalifu wa vijana kutokana na tukio hilo lililotokea mwezi uliopita.
Kwa mujibu wa wapelelezi, Jeanine alifanya ngono na wavulana wawili wenye umri wa miaka 17 na 13 mnamo Machi 11 ndani ya nyumba moja mjini Sarasota wakati wa Mapumziko ya majira ya Kiangazi.
Kijana mwingine wa kiume na wasichana wawili ambao pia walikuwa kwenye nyumba hiyo waliwasikia na wakati fulani walishuhudiwa vitendo vya ngono vikifanyika, kwa mujibu wa maofisa wa usalama.
Mwanamke huyo mwenye miaka 42 pia alidaiwa kununua chumba mbili za pombe ya vodka zenye ladha ya keki kwa ajili ya vijana hao, kwa mujibu wa hati ya kukamatwa kwake iliyopatikana.
Pia iliripotiwa kwamba Jeanine alidaiwa kuwatishia kukodi muuaji kumuua yeyote ambaye atasimulia kilichotendeka kati yake na watoto hao.
Anashikiliwa kwa dhamana ya jumla ya Dola za Marekani 100,500, imeripotiwa. Mashitaka yake yamepangwa kusikilizwa Mei 11.
Kwa mujibu wa ukurasa wake wa Facebook, Jeanine, mwenye asili ya Bronx, New York, ameolewa na anafanya kazi kama mtunzaji mikono na kucha.
Mumewe aliyeishi naye kwa zaidi ya miaka mitatu, Tom Shimandale, alieleza kwamba anaona giza totoro kuhusu kukamatwa kwa mke wake.
"Nimechanganyikiwa sifahamu kinachoendelea. Nimeshitushwa na nimehuzunishwa," alisema. "Unadhani unamfahamu mtu fulani."
Shimandale alisimulia hayo alipokutana na mkewe jela kufuatia kukamatwa kwake, mwanamke huyo hakujisumbua kumwomba msamaha kwa usaliti huo, lakini alimwomba amwekee dhamana ili aachiwe kwa fidia ya talaka.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item