MBARONI KWA KUFANYA MAPENZI NA BINTI YAKE WA KUMZAA MBEYA...
https://roztoday.blogspot.com/2013/04/mbaroni-kwa-kufanya-mapenzi-na-binti.html
Polisi mkoani Mbeya inamshikilia mwanaume mmoja kwa kosa la kufanya mapenzi na mwanawe wa kumzaa.
Anayeshikiliwa ni mkulima na mkazi wa kijiji cha Syukula wilayani Rungwe Asajile Mwamtina(46) ambapo anatuhumiwa kufanya tukio hilo Aprili 14 mwaka huu.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Barakael Masaki alisema saa 12:00 za jioni Asajile alimvizia mwanawe wa kumzaa mwenye umri wa miaka 13 aliyekuwa jikoni akiendelea kupika na kisha kumshawishi kufanya naye mapenzi.
Alisema bila kujali utu na heshima aliyopaswa kuonesha kwa binti yake, baba huyo alifanikiwa kufanya mapenzi na mwanawe anayetajwa kuacha shule mwaka 2011 akiwa darasa la tano kutokana na ugonjwa wa kifafa unaomsumbua.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda Masaki, wakati hayo yakiendelea mke wa mtuhumiwa ambaye ndiye mama mzazi wa binti huyo, Tumikigwe Samalinga alikuwa safarini katika kijiji cha Kiwira wilayani Rungwe kuuguza mgonjwa ambaye haijafahamika mara moja ni nani katika familia hiyo.
Kutokana na tukio hilo, kamanda ameitaka jamii kuacha tamaa mbaya za kimwili na kujiletea fedheha kwa jamii sanjari na kufikishwa katika mkono wa sheria.
Wakati huo huo, vitendo vya kinyama dhidi ya watoto vimeendelea kuibuka baada ya mkoani Mwanza, mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu kuuawa na watu wasiojulikana na kisha kukatwa ulimi, mkono, mguu wa kushoto na kisigino cha mguu wa kulia na kuondoka navyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ernest Mangu alisema mauaji hayo yamefanyika Aprili 16, mwaka huu saa 4.30 asubuhi katika kisiwa cha Maisome kijiji cha Kisaba, kitongoji cha Lwabatele.
Mtoto huyo, Erick Msoma alipotea nyumbani kwao tangu Aprili 10, mwaka huu katika kijiji cha Kahunda, kata ya Katwe wilayani Sengerema kabla ya kubainika akiwa ameuawa. Polisi inaendelea na upelelezi kubaini wahusika ili hatua za kisheria zichukuliwe.