KAMERA ZA CCTV ZANASA MZIMU UKIRANDARANDA DUKANI USIKU...

Video inayoonesha tukio zima la vitu vikiangushwa dukani humo huku kukiwa kumefungwa usiku wa manane.

Duka moja kubwa lililoko Australia Kusini limeeleza kuwa wapelelezi wa viumbe visivyo vya kawaida wanachunguza uwezekano wa kuwapo mzimu ndani ya jengo la duka hilo.
Mmiliki wa duka hilo la Brompton IGA, Norm Hurst amesema amekuwa akifuatilia nyendo za mzimu huo baada ya kugundua kasha la matunda likiwa limehama takribani mita sita kutoka lilipokuwa awali baada ya kuwa tayari ameshafunga duka.
“Siku zilizopita nihisi kuna mzimu unanifuatilia,” Hurst aliliambia gazeti la Adelaide Now. “Nafikiri, ndio, kwa vyoyote.” Lakini tangu ninunue jengo hili, mambo ya ajabu yamekuwa yakitokea.”
Hurst alipofuatilia kamera za CCTV, alishitushwa na alichokiona.
“Moja ya kamera zilionesha moja ya ganda la pakiti za chokoleti likidondoka chini,” amelieleza gazeti la Herald Sun. “Halikupeperushwa tu, bali imetupwa. Chokoleti hizo zimepangwa mita 12 kutoka hapo lilipodondokea.
Kona mbalimbali za kamera hizo zinaonesha hakuna mtu yeyote jirani wakati tukio hilo la kushangaza linatokea.
Hurst amesema dukani kulikuwa hakuna mtu, pamefungwa na ilikuwa muda mfupi kabla ya usiku wa manane ndipo tukio hilo lilitokea.
Baadhi ya watazamaji wa video hiyo wameitoa dosari kwa kusema muda umeonekana umechakachuliwa kabla ya bidhaa kuanza kuonekana, kutoka saa 5:27 usiku hadi saa 5:30 usiku, wakishutumu kuwa video hiyo imehaririwa.
Mmoja alihoji, ingawa kamera hizo hutegwa kurekodi mara zinapohisi kitu kinachoendelea, unahitajika ufafanuzi wa tofauti hiyo ya dakika tatu katika muda uliooneshwa kwenye video.
Alhamisi usiku, duka hilo liliripoti wapelelezi wa viumbe visivyo vya kawaida wamewasili kuchunguza duka hilo.
Mpelelezi mmoja, Jessica Pulvirenti, aliliambia gazeti la Metro, ameitazama na kuitathmini video na ameridhika kuwa ni halisi wala haikuchakachuliwa.
“Nadhani ni halisi kabisa, kwa hakika,” alisema Hurst akihojiwa na gazeti la Metro.
“Mzimu hakuleta madhara yoyote,” alisema alipokuwa akifafanua sababu za kuamini hizo na kuongeza “mzimu ulikuwa na meno mazuri.”

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item