MAAJABU!! MAITI ILIYOZIKWA MIAKA 130 YAKUTWA KAMA YA JUZI...


JUU KUSHOTO: Askari wakikagua kaburi baada ya ya wizi kutokea. JUU KULIA: Mwili wa marehemu huku nywele ndefu zikionekana kwa nyuma. CHINI KUSHOTO: Kibao kinachoonesha mwaka aliozikwa marehemu. CHINI KULIA: Mdomo ulioachama huku meno yakionekana.

Vijana kadhaa wanaosadikiwa kuwa ni wezi, wamevunja na kuiba vitu kadhaa kwenye kaburi alimozikwa mama mmoja miaka 130 iliyopita nchini China.
Hilo ni mara ya pili kwa kaburi hilo kuvunjwa na wezi, kwani mara ya kwanza ilikuwa miaka ya 1950 ambapo wezi walivunja lakini wakaingiwa na roho ya kibinadamu kwa kutochukua chochote wala kumpekua marehemu huyo.
Katika tukio la hivi karibuni, wezi hao wanaosadikiwa kuwa wanne walipatwa na mshangao mkubwa baada ya kukuta mwili wa marehemu huyo ukiwa kama umezikwa juzi.
Tofauti na ilivyo kawaida kwa mtu aliyekaa ardhini kitambo, mwili huo ulionekana ukiwa bado una ngozi yenye hali nzuri, nywele ndefu zilizoshuka hadi mgongoni na mdomo wake uliokuwa umeachama kidogo ukiacha wazi meno.
Mama huyo alizikwa kwenye makaburi ya familia yaliyoko mjini Ningde, Jimbo la Fujian. Juu ya kaburi hilo palisomeka kuwa amezikwa mwaka 1882.
Vitendo vya wizi makaburini vimeshika kasi nchini humo licha ya juhudi za serikali na polisi  kukomesha vitendo hivyo, ambapo sasa wezi hao wamefikia hatua ya kutumia tingatinga na baruti kurahisisha kazi yao.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item