ASILI YA MAJINA YA MAENEO MBALIMBALI...

Moja ya majengo ya serikali yaliyopo katika eneo la Kiponzelo, mkoani Iringa.
Kiponzelo ni moja ya maeneo maarufu katika mkoa wa Iringa. Lakini naamini wengi hawafahamu asili ya jina hili. Kaa chini nikupe simulizi ambayo hatimaye ikazaa jina la Kiponzelo. Wakati wa upanuzi wa barabara kuu iendayo Zambia ambayo inapita katika mkoa wa Iringa, mzungu mmoja akiwa sambamba na Waswahili kadhaa walikuwa makini wakichukua vipimo kadhaa kwa kutumia mashine zao. Ikafika wakati wakiwa kwenye eneo ambalo sasa linajulikana kama Kiponzelo, Mzungu akasimama upande mmoja huku akiangalia kwenye kamera yake maalumu kwa upimaji na Mswahili mmoja akiwa na fimbo yake maalumu kwa kazi hizo akipokea maelekezo kutoka kwa Mzungu. "Keep On Zero! Hey, Keep On Zero," alipiga kelele yule Mzungu mara kwa mara akimaanisha Mswahili achomeke ile fimbo mahali inaposomeka Sifuri! Wakati wakiendelea hivyo, ndipo Mnyalu mmoja akakatiza akielekea kilabuni na kusikia yale maneno. Bila hiyana akayafikisha kwa washikaji wake kwamba kamuona Mzungu Kiponzelo, akimaanisha lile eneo walipokuwa wakifanya upimaji. Nakutakieni siku njema...

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item