UJEURI NA KIBURI CHA DENNIS RODMAN WAFIKIA TAMATI...
https://roztoday.blogspot.com/2012/05/ujeuri-na-kiburi-cha-dennis-rodman.html
Ujeuri na kiburi cha mwigizaji na mchezaji mpira wa kikapu nyota, Dennis Rodman umefikia ukingoni pale alipochimbiwa mkwara mzito, "kama hautafanya Jaji atakushukia kama nyundo."
Jaji wa Mahakama ya Orange County alikuwa akisikiliza kesi ya madai dhidi ya Rodman kukwepa kulipia fedha kiasi cha Dola za Marekani 808,935 za kusaidia matunzo ya watoto wake wawili, mmoja wa miaka 9 na mwingine 10, na ziada ya malimbikizo Dola za Marekani 51,441.
Rodman amewekwa chini wa uangalizi wa miaka mitatu na kuamriwa kufanya kazi za kusaidia jamii jumla ya masaa 104.
Wakati akiwa chini ya uangalizi, Rodman anatakiwa kuwa karibu na malezi ya watoto hao na kugharimia mahitaji yao. Haikuwekwa wazi jinsi atakavyotumikia adhabu hizo.
Siku zilizopita Rodman alijibu madai hayo ya mke wake wa zamani, Michelle kwa kusema hawezi kulipa sababu walikwishatengana.
Kwa mujibu wa Dennis, madai Michelle yanahusisha amri ya malipo ya Dola za Marekani 50,000 kila mwezi kwa ajili ya matunzo ya watoto aliyokuwa akidai.
Rodman amekuwa akipambana tangu mwana 2010 kupinga hilo.
Ni dhahiri kwamba, Jaji hakununua kile alichokuwa akiuza Dennis!