CHEKA TARATIBU...
https://roztoday.blogspot.com/2012/06/cheka-taratibu_12.html
Mlevi mmoja mcha Mungu akiwa bado na mipombe yake kaamkia kanisani Jumapili moja.
Kama ilivyo kawaida ya misa, kuna nyakati waumini hutakiwa kusimama na pengine kukaa. Zoezi hilo kwa mlevi likawa ni adhabu kwake na hivyo kuamua kukaa ndipo usingizi ukampitia.
Mchungaji wakati akianza hadi anamaliza mahubiri akamuona jamaa hajitambui kwa usingizi, ndipo akaamua kuhakikisha kama anafuatilia misa au la.
Mchungaji akasema, "Walio tayari kwenda peponi wasimame!" Kanisa zima wakasimama isipokuwa yule mlevi. Akarudia tena kwa sauti ya juu zaidi, "Walio tayari kwenda peponi wasimame!" Kwa bahati safari hii mlevi akasikia na kuanza kujizoazoa kizembe wakati wengine wakikaa kiasi cha kujikuta kasimama peke yake.
Huku akiwa kachanganyikiwa akasema, "Sifahamu hapa tunapigia kura kitu gani, Mchungaji, lakini haina ubishi kwamba wewe na mimi pekee ndiyo tumesimama kwa ajili yake!" Duh, ulevi noma...