CHEKA TARATIBU...

Waumini zaidi ya elfu mbili wamejaa kanisani katika ibada ya Jumapili. Mchungaji akiwa tayari kuanza ibada, mara vijana wawili wakaingia kupitia mlango wa mbele wakiwa wamevalia makoti meusi huku mikononi wakiwa wameshika bunduki.
Wakati kila mmoja mle ndani akiwa kapigwa butwaa, wale vijana wakauliza kwa sauti, "Kila mmoja ambaye yuko tayari kupigwa risasi kwa ajili ya Yesu abaki kwenye kiti chake!"
Kusikia hivyo mabenchi karibu yote yakabaki matupu wakifuatiwa na wanakwaya. Mara Shemasi naye akatimua mbio akifuatiwa na Kiongozi wa kwaya na Mchungaji msaidizi.
Baada ya dakika kadhaa, wakabaki kama watu ishirini wameketi kwenye viti kanisani. Mchungaji alikuwa bado kabaki palepale madhabahuni.
Vijana wale wakaweka silaha zao chini na kumwambia Mchungaji, "Sawa, Mtumishi wanafiki wameshaondoka. Unaweza kuendelea na ibada." Duh, imani kazi kwelikweli...

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item