CHEKA TARATIBU...
https://roztoday.blogspot.com/2012/06/cheka-taratibu_4157.html
Padri na Dereva Teksi wote wamwkufa na kwenda peponi. Mtume Petro alikuwa kwenye lango kuu akiwangojea. Akamwambia Dereva Teksi, "Nifuate." Akafanya kama alivyoambiwa na kumfuata Petro hadi kwenye jumba kubwa. Lilikuwa na kila kitu unachofikiria pamoja na bwawa la kuogelea.
"Nashukuru sana Mtume," alisema Dereva Teksi kwa furaha.
Kisha, Mtume Petro akamchukua Padri kwenye kijumba chakavu, kitanda kibovu na televisheni ndogo ya zamani.
"Subiri, nafikiri kuna mkanganyiko kidogo hapa", alisema Padri. "Mimi ndio nilistahili kupewa jumba kubwa. Licha ya hivyo nilikuwa Padri, nakwenda kanisani kila siku, na kuhubiri neno la Mungu."
Mtume Petro akajibu, "Ndio, hiyo ni kweli kabisa. Lakini wakati wote unapohubiri waumini wako walikuwa wakilala. Wakati Dereva Teksi aliwaendesha kila mmoja aliyesali."