FAMILIA YAHAHA KUSAKA FEDHA ZA MAZISHI YA RODNEY KING...

Rodney King hakuwa mtu tajiri wakati akifariki...na sasa familia yake inaomba jamii kuchangia fedha zitakazowezesha nyota huyo kupata maziko yanayostahili, imeelezwa.
Licha ya ukweli kwamba Rodney amepata fidia ya Dola za Marekani milioni 3.8 kutoka Jiji la Los Angeles baada ya tukio la mwaka 1992, familia yake imeeleza kuwa hakuna fedha yoyote iliyosalia kulipia gharama za mazishi yake, ambayo yanakisiwa kufikia zaidi ya Dola za Marekani 22,000.
Familia yake sasa imetoa taarifa kupitia kwa mwakilishi wao, Kali Bowyer, aikiomba watu kuchangia mfuko maalumu wa mazishi ulioanzishwa kwa jina la 'wote wenye nia ya kuchangia familia ya King.'
Mabinti watatu wa Rodney, sambamba na wanafamilia wengine, wanahaha kupata fedha...lakini Bowyer amesema, "Wanahitaji fedha."
Rodney anatarajiwa kuzikwa Juni 30, mwaka huu.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item