JAMAA WA PARKING AMRUNDIKIA TIKETI MGONJWA HOSPITALINI...
https://roztoday.blogspot.com/2012/06/jamaa-wa-parking-amrundikia-tiketi.html
Msimamizi wa maegesho ya magari 'mwenye ari kubwa' amebandika tiketi kumi katika gari lililoegeshwa kwenye eneo la walemavu la hospitali wakati mmiliki wake akiwa anafanyiwa upasuaji wa dharura.
Tiketi hizo zilibandikwa sehemu kubwa ya kioo cha mbele cha gari hilo dogo jekundu na msimamizi huyo baada ya mgonjwa kuegesha katika eneo hilo.
Asingeweza kuondoa gari kufuatia upasuaji huo wa dharura, lakini uwekaji tiketi huo umefanyika licha ya kuweka alama ya bluu ikimtambulisha kwamba ni mlemavu na kueleza kwamba amefika kwa ajili ya kupandikizwa ini.
Maofisa wa Kampuni ya Maegesho walilazimika kufanyia kazi tuhuma hizo baada ya kushutumiwa vikali na wagonjwa, wageni na wanasiasa kufuatia hatua hiyo kinyama.
Mtu mmoja alisema: "Ni kukosa fadhila, uko wapi ubinadamu?"
Mwanamke huyo mgonjwa ambaye hatutajwa jina, aliegesha gari hilo kwenye eneo la walemavu katika Hospitali ya Chuo Kikuu, Cardiff nchini Wales alikokwenda kubadilishwa figo yake.
Lakini baada ya dharura alilazimishwa kukaa hospitalini na hakuweza kuliondoa gari lake eneo hilo.
Tiketi hizo kumis, kila moja ikilipiswa Pauni za Uingereza 30 zilibandikwa mbele ya kioo chake cha gari katika matukio kumi kuanzia Mei 16 hadi mwishoni mwa wiki iliyopita.
Zilibandikwa hapo licha ya kuwekwa karatasi maalumu ndani ya gari hilo, kando tu ya kibali cha kutambulisha ni mlemavu, kinachosema mmiliki alikuwa ni mgonjwa katika kitengo cha upandikizaji cha hospitali hiyo.
Wageni wengine walimshambulia msimamizi huyo aliyeajiriwa na kampuni binafsi ya Vinci Park UK. Andrew RT Davies, kiongozi wa Chama cha Conservative cha Wales, wakimtaka kuwa na 'ubinadamu'.
Alisema: "Wakati nikifahamu sheria za maegesho na utekelezaji wake ni muhimu, siwezi kusaidia lakini nafikiri kwa mfano huu haiondoi nafasi ya kutumia ubinadamu.
"Kukatisha tiketi 10 ni zaidi ya uwajibikaji, kusema kwa uchache.
"Wakati unafahamu kila mmoja anayetumia maegesho ya hospitali anakuwa tayari yuko kwenye msongo kiasi fulani wa mawazo, ubinadamu kidogo unahitajika kuoneshwa kwenye kutoza faini ya maegesho.
Mmiliki wa gari hilo dogo la mwaka 2009 jana alikuwa akiendelea kupata nafuu hospitalini baada ya upasuaji. Mgeni mmoja alisema:
"Nakereka sana kufikiri kwamba msimamizi wa maegesho ya magari hakuweza kuonesha ubinadamu wowote.
"Hivi wanajua kweli athari zinazoweza kutokea kwa mtu ambaye ndio ametoka tu kwenye upandijizwaji ini? Inaonekana kama vile hawajali kabisa."
Ruth Walker, Mkurugenzi wa Uuguzi katika Bodi ya Afya ya Chuo Kikuu Cardiff na Vale amesema: Tunaongea na kila mmoja aliyehusika kujaribu kupata ufumbuzi wa tukio hili.
Msemaji wa kampuni ya Vinci Park UK alisema: "Masharti yetu na vigezo vimeelezwa wazi kwenye mashine za tiketi.
"Tunaweza kuhakikisha taarifa za gharama za maegesho zimeondolewa kutoka kwenye gari na tunafanya kazi kwa kushirikiana na Bodi ya Afya ya Chuo Kikuu cha Vale kupatia ufumbuzi tatizo hili."