JANJA YA MAMA WA WHITNEY KUHUSU KITABU YAGUNDULIKA...
https://roztoday.blogspot.com/2012/06/janja-ya-mama-wa-whitney-kuhusu-kitabu.html
Mpango wa mama wa mwimbaji Whitney Houston kutoa kitabu kuelezea maisha ya mwanae huyo, umepingwa vikali na wanafamilia ambao wamedai kuwa ni janja yake kutaka kuchuma pesa za chap chap kupitia mwanae.
Mama huyo Cissy Houston amepanga kuchapisha kitabu kupitia kampuni ya Harper Collins akidai ni katika kumuenzi mwanae, lakini baadhi ya wanafamilia wamefichua kwamba ni mbinu zake tu za kutaka kujipatia fedha baada ya Whitney kumrithisha kila kitu binti yake, Bobbi Kristina.
Kitabu hicho ambacho kimepangwa kuwa mitaani mwakani, kimepigwa vita na wanafamilia ambao wameongeza kuwa, Cissy anataka kukitumia pia kujipigia debe aonekane kama 'mama bora duniani, wakati kiuhalisia hastahili."