JASUSI ALIYETUNGUA NDEGE LOCKERBIE AFA KWA SARATANI...

JUU KUSHOTO: Abdelbaset Ali Al-Megrahi akiwa amelala kitandani baada ya kuwa amepata kansa ya kibofu wakati akitumikia kifungo cha maisha baada ya mauaji ya kikatili ya mwaka 1988. JUU KATIKATI: Picha za hivi karibuni zikimwonesha mlipuaji huyo akiwa amesawajika kabisa kutokana na kansa iliyokuwa imeenea mwilini mwake. JUU KULIA: Eneo ambapo ndege hiyo ilianguka. CHINI KUSHOTO: Mabaki ya ndege hiyo eneo la ajali. CHINI KATIKATI: Sehemu walipozikwa watu waliokufa katika ajali hiyo ya ndege. CHINI KULIA: Kasri ambamo Abdelbaset alifia kutokana na maradhi ya kansa ya kibofu.
Mtu huyo mwenye umri wa miaka 60 alipata maradhi ya kansa ya kibofu wakati anatumikia kifungo cha maisha jela, kutokana na kitendo cha kikatili cha mwaka 1988 kilichoteketeza watu 270.
Aliachiwa baada ya madaktari kusema kuwa al-Megrahi alikuwa na miezi mitatu tu ya kuishi, hatua iliyoamsha hasira miongoni mwa wanafamilia wa waathirika, kuwa kuachiwa kwake kulifanywa ili nchini hiyo (Uskochi) iweze kuwa na uhusiano mwema na Libya - nchi yenye utajiri mkubwa wa mafuta.
Alipata mapokezi ya kishujaa alipowasili katika jiji la Tripoli na kutembezwa katika mitaa ya jiji huku akifuatana na Saif, mtoto wa Kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi.
Al-Megrahi, aliyekuwa jasusi wa Libya, alifariki kitandani nyumbani kwake Tripoli huku akiwa amezungukwa na wanafamilia yake.
Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, akizungumzia kifo cha Al-Megrahi alisema: 'Leo ni siku ya kukumbuka watu 270 waliopoteza maisha yao kwa kile kinachoitwa vitendo vya kutisha vya kigaidi.'
Jim Swire, ambaye binti yake Flora aliuawa wakati ndege ilipotunguliwa, alisema 'hakupendezwa hata kidogo' na habari za kifo cha Megrahi.
Dr Swire, mmoja wa watu wanaounda kundi la Justice for Megrahi (JFM), anaamini kuwa lazima kuwepo na ushahidi utakaothibitisha kuwa Megrahi hakuwa na hatia.
'Kifo cha Megrahi si habari njema,' aliiambia televisheni ya Sky News. 'Nilikutana naye uso kwa uso jijini Tripoli Desemba mwaka jana, alipokuwa akiumwa sana na kuonekana mtu mwenye maumivu makali.
'Lakini bado alitaka kuzungumza nami kuhusu taarifa walizokusanya akiwa na timu yake ya ulinzi ambazo angelitaka niletewe baada ya kifo chake.
'Nadhani hilo ni jambo la kushangaza kufanywa na mtu aliyefahamu fika kuwa anakufa.'
Dk Swire aliongeza: 'Hadi mwisho alikuwa amenuia - kwa ajili ya familia yake, japo alijua alikuwa amekwisha chelewa, lakini kwa ajili ya familia yake - kuonyesha jinsi hukumu dhidi yake alivyotaka ipinduliwe.
'Na pia alifanya hivyo kwa ajili ya ndugu wengine waliofikia uamuzi baada ya kuusoma kwa makini ushahidi kuwa hakuwa na hatia, na nadhani hilo ndilo litakalotokea.'
The Wizara ya Mambo ya Nje na Halmashauri ya Mji wa East Renfrewshire wanasema wanachunguza taarifa zinazohusu kifo chake.
Martin Cadman, kutoka mji wa Norfolk, ambaye mwanawe naye alifariki katika ndege ile akiwa na umri wa miaka 32, alisema: 'Kitu pekee kinachonifurahisha mimi ni katika kupata ukweli. Wamarekani wanaufahamu zaidi kuliko hata walivyoeleza awali'.
David Ben-Ayreah, msemaji wa Waingereza walioathirika, alimwelezea Megrahi: "Nilifahamishwa katika siku saba zilizopita kutoka chanzo cha kuaminika mjini Tripoli kuwa Megrahi alikuwa katika hali mbaya ya kufikia hadi kuzimia, kwamba alikuwa pia na matatizo ya tumbo na sehemu za chini ya kifua, na kwamba aliongezewa damu karibu mara tatu,' alisema.
'Watu watakisikitikia sana kifo chake. Mimi nikiwa miongoni mwa watu walihudhuria kesi yake, siamini kuwa Megrahi alikuwa na hatia.'
Pamela Dix, alimpoteza kaka yake, Peter (35) katika ajali ile na sasa alidhani hatajua nini hasa kilichotokea.
Bi Dix (54), kutoka Woking, Surrey, alisema: 'Kifo cha Megrahi ni kama kimefunga mlango. Anakufa akiwa mtu aliyetiwa hatiani huku akiwa ni kama ufunguo wetu wa kupata ufumbuzi wa kilichotokea na sasa ametoweka, kitu kitakachotufanya tusipate fursa tena ya kumsikia.'
Alisema; 'Itakuwa si sawa.'
'Kukiwa na usia mzuri hapa. duniani - au tupate mtu kama waziri mkuu wa Uingereza - ambaye atakwenda kwa undani, japo hafanyi hiyo, unaweza kufanya mengi.
'Kama ungeniambia miaka 23 iliyopita vita ambayo tungekutana nayo katika mfumo wa kesi za jinai, si mawaziri wakuu wala hata mawaziri wa mambo ya nje wamelioshindwa, sina uhakika mimi ningefanya nini.
'Wakati mwingine ile hofu ya kilichotokea Lockerbie kinafanya hata kusahau kilichowapata wale watu 270. Tunajikuta tukiwa tumetoka mbali na kukiona kama kitu cha ajabu na kushangaza.
'Megrahi ndiye aliyekuwa mhusika mkuu lakini kwa vile ameshakufa, sasa tujadili nini hasa ndiyo jambo husika - kitu gani kilichoipata ndege ya Pan Am 103?'
JFM, chombo kinachowakilisha familia za waathrika, ambao si rahisi kuwashawishi vinginevyo kuhusu kuhusika kwa Megrahi kwa ulipuaji ule, kimeamua kukata rufani ili kesi ifunguliwe upya.
Eileen Monetti, raia wa Marekani, aliyempoteza mwanawe wa miaka 20 katika ulipuaji ule, alisema hana haja ya kusherehekea kifo cha Megrahi.
Akizungumza kutoka nyumbani kwake New Jersey, alisema: 'Niliposikia kwa mara ya kwanza nilitaka kumhoji aliyeniambia
'Sasa Megrahi atakutana na Mungu wake na kupewa hukumu yoyote iwayo. Sina nafasi ya kumhukumu lakini nadhani haitayabadilisha maisha yangu kwa kiasi chochote, maana hadi kufikia hapo atakuwa ameyabadili kwa kiasi kikubwa maisha yangu.
Wafanyakazi wa kliniki binafsi jijini Tripoli, Libya, alikopelekwa kuongezewa damu walisema alikuwa na
'Alizimia na kukupoteza fahamu mara baada ya kuongezewa damu na huenda asiamke tena,' kilisema moja ya vyanzo hivyo.
Rafiki wa karibu wa familia hiyo alithibitisha matatizo aliyonayo kwa kusema hali ya Al-Megrahi imezidi kuzorota kwa kiasi kikubwa katika siku tatu zilizopita.
Al-Megrahi alikuwa katika kliniki ya Al-Afia iliyopo kilometa chache tu kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Tripoli, alikopokewa kwa shangwe mwaka 2009 baada ya kuachiliwa akitokea Uingereza, kwa misingi ya huruma kwa sababu tu alikuwa na kansa ya kibofu.
Kabla ya kifo chake iliripotiwa kuwa kansa ya kibofu ilikuwa imeenea hadi shingoni. Wengine walisema kilichomsaidia ni kutumia dawa za kansa ambazo hazikuwa zikipatikana nchini Uingereza.
Mbali na kuleta utatanishi wa kimataifa, na kura iliyoashiria kutupwa kwa uamuzi wa Bunge la Uskochi, kuachiwa kwa Megrahi kutoka jela hakuonekani kuwa kulichochewa na chama cha SNP ili kifadhiliwe.
Chama hicho kikiongozwa na MacAskill, kilirejeshwa madarakani mjini Holyrood katika ushindi wa kishindo Mei mwaka uliopita.
Kiongozi wa Chama cha Labour cha Scotland, Johann Lamont, alikitaja kitendo cha kumwachilia Megrahi kama
'Kwa sasa, naomba, kwa niaba ya watu wa Scoltand, kuomba radhi kwa familia za waathirika wote wa mlipuko wa Lockerbie kwa kuachiliwa kwake mapema,
Kiongozi wa chama cha Uskochi cha Liberal Democrats, Willie Rennie, alisema: 'Japokuwa huu ni kama mwisho wa masuala mabaya zaidi ya nchini Scotland, hakuna haja ya kusherehekea kwa kuwa Abdelbaset al-Megrahi ameshafariki.
'Badala yake kiwe kama kichocheo cha kuhimiza kupatikana kwa ukweli, ikiwa ni pamoja na ushahdi muhimu wa mahakama uliokubalika katika kesi.'
Ilikuwa ni aghalabu kumuona Megrah tangu aliporejea Tripoli, alikuwa akionekana katika matangazo ya televisheni kwa kile kilichoonekana kama maandamano ya kiserikali yaliyofanyika Julai.
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, William Hague, alisema kuonekana hadharani kunathibitisha 'kosa kubwa.'
Kifo cha Megrahi kitaashiria mwisho wa vita ya muda mrefu ya ndugu wa familia ya waathirika, iliyomfanya mtu huyo aliyekuwa jasusi kukumbana na mkono wa sheria nchini Marekani.
Megrahi alikuwa mtu pekee aliyehukumiwa mwaka 2001 katika kesi ya ulipuaji wa ndege ya shirika la ndege la Pan Am 103 mwaka 1988, wakati ilipokuwa ikisafiri kutoka London kwenda New York.
Abiria wote 259 waliokuwamo katika ndege hiyo waliteketea ikiwa ni pamoja na wengine 11 walioangukiwa na mabaki ya vipande vya ndege hiyo katika mji wa Lockerbie.
Baada ya mvutano wa kimataifa wa muda mrefu, Megrahi alishitakiwa katika mahakama hiyo ya Camp Zeist, kwa kufuata sheria za Kiskochi. Alionekana na hatia kwa mauaji ya halaiki mwaka 2001 na kuhukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 27 jela.
Mbali na malalamiko kuwa hakuwa ametenda jambo hilo akiwa peke yake, na baadhi ya watu kumuona kuwa hakuwa na hatia, Megrahi alikuwa mtu pekee aliyewahi kuhukumiwa kwa shambulio la kigaidi.
Aliachiwa kutoka jela baada ya kutumikia karibu miaka minane ya kifungo chake, alipotupilia mbali rufani yake ya pili akipinga hukumu hiyo katika mahakama ya rufani ya Edinburgh.
Uamuzi wa jaji wa Mahakama ya Uskochi, Kenny MacAskill, wa kuruhusu Megrahi kurudishwa kwao Libya, uliamsha shutuma nyingi kutoka kwa familia ya waathirika na wanasiasa, wakitaka arejeshwe jela.
Familia za Wamarekani ndiyo waliopigia kelele sana uamuzi huo, akiwamo Rais wa Marekani Barack Obama na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton wakiishutumu hakumu hiyo kwamba ilitolewa 'kimakosa kabisa'.
Chuki ya Wamarekani kuhusu uamuzi huo ilichagizwa na Megrahi kupokewa kishujaa alipowasili Tripoli.
Susan Cohen, ambaye binti yake Theodora (20) alikuwa katika ndege hiyo ya Pan Am 103 iliyokuwa ikielekea Uwanja wa ndege wa John F Kennedy, alisema ni bora kama Megrahi angelihukumiwa adhabu ya kifo.
Akizungumza kutoka nyumbani kwake Cape May Court House, New Jersey, Bi Cohen (74), alisema: 'Megrahi alikufa akiwa amezungukwa na familia yake wakati binti yangu alikufa kifo kibaya alipokuwa na umri wa miaka 20 akiwa na matarajio kibao maishani mwake. Je, unaweza kuuita hiyo haki?
'Simuonei huruma hata kidogo, ni bora kama angelikufa mapema zaidi. Huyu alitakiwa ahukumiwe Marekani na kupewa adhabu ya kifo. Kumwangalia akiachiwa hivi hivi kutoka jela iliniuma sana.'
Bi Cohen alisema maswali bado yanabaki jinsi ulipuaji ulivyofanyika na nani walihusika katika ajali ile iliyompoteza binti yake, mwanafunzi aliyekuwa akitarajia kuwa mwigizaji.
'Nadhani haya yalikuwa ni makubaliano ya kijinga yanayopaswa kudharauliwa. Hatuwezi kuacha kifo cha Megrahi kiwe kikwazo kwa serikali za Marekani na ya Uskochi, kutafuta nani alihusika na ulipuaji na jinsi hasa ulivyofanywa.
'Sikubaliani kabisa na habari za njama kwamba Megrahi hakuwa na hatia.'
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron naye amepata shinikizo kutoka kwa baadhi ya maseneta wa Marekani, wakitaka kuundwe tume ya uchunguzi kuhusu uamuzi wa kumwachia huru mlipuaji.
Hata hivyo, hatua hiyo iliungwa mkono na ndugu wa waathirika walio Uingereza na watu maarufu kama Nelson Mandela na Askofu Desmond Tutu.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton pia ametaka kuundwe tume ya uchunguzi, huku kukiwa na madai kuwa kampuni ya mafuta ya BP ilishawishi aachiwe huru ili wapate mikataba minono ya Libya.
Pia iliibuka mwaka uliopita kuwa waziri mkuu mstaafu wa Uingereza, Tony Blair alikuwa na mazungumzo ya siri na Kanali Gaddafi miezi michache kabla ya Megrahi kuachiwa, kutokana na barua na pia barua pepe zilizoibuliwa katika mji uliokumbwa na vita wa Tripoli.
Katika safari zake za Libya wakati fulani, Blair alifuatana na mfanyabiashara bilionea wa Kimarekani. Inasemekana Walibya walitaka kuzungumzia makubaliano ya kujenga eneo la mapumziko la ufukweni.
Lakini mbali na kukubali kuwa Gaddafi aliwahi kuzungumzia suala la Megrahi, Blair akikataa katakata kuwa na jambo lolote kuhusu kuachiwa kwake, akisema kuwa mara zote suala hilo lilikuwa mikononi mwa uongozi wa juu wa serikali ya Uskochi.
Tangu mwanzo Megrahi mwenyewe alikuwa akitetea kutokuwa na hatia. Alipotimiza miaka 60 ya kuzaliwa Aprili mosi, alisali kumuomba Mungu kutokee
Alijaribu kufanya sala hizo huku akiwa kitandani, akidai kuna mbalimbali mambo yaliyoendeshwa vibaya.
Kitabu hicho kiliegemea ushahidi ambao haukupata kusikika, alitaraji kuutoa katika rufani ambayo hata hivyo hakuitekeleza. Alidai alikuwa akipewa shinikizo na MacAskill kuondoa refani ili aweze kurejeshwa Libya
Alipowasili Libya, Megrahi alipokewa kishujaa na utawala wa Kanali Gaddafi na serikali mpya ya mpito ilikataa kumkabidhi kwa Marekani ili akakabiliane na mashitaka zaidi.
Chanzo kilicho karibu na familia ya Megrahi kilisema: 'Alikuwa akionekana kama Mlibya aliyehukumiwa kimakosa na kutiwa hatiani kimakosa kama gaidi.
'Kaka Abdelbaset alikuwa akiungwa mkono sana bila kujali mahusiano aliyokuwa nayo na Gaddafi. Kwa Abdelbaset, Walibya wengi walikuwa wanamuona kama shujaa wa taifa.'
Maisha yake yalirefushwa na aina mpya ya dawa ya kansa iliyogunduliwa London ambayo bado haijapatikana sana nchini Uingereza. Dawa ya Abiraterone, yenye thamani ya paundi 3,000 za Uingereza kwa mwezi, ikiwa na dawa zenye virutubisho, iligunduliwa na katika Taasisi ya Utafiti wa Kansa.
Familia yake wameapa kukata rufani upya kwa niaba yake baada ya kifo chake.
**Imetafsiriwa na Bakari Omari Bakari 'Teacher' - +255 655 188666

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item