KUTANA NA MAGAIDI KATILI ZAIDI KUTOKA IRAK...

Magaidi hao wakijiandaa kuchinja mmoja wa mateka. PICHA NDOGO KULIA: Norman Kember (juu) na Margaret Hassan.
Ni dhahiri waliuawa bila hofu, bila hila zozote kukamatwa na vikosi maalumu katili zaidi duniani.
Hakuna kinachoonekana kuweza kuzuia magaidi wawili wakuu wa kundi la Al Qaeda nchini Irak wakiongoza kampeni ya matukio ya utekaji nyara wa viongozi wakuu, kulipua magari kwa mabomu na mauaji mjini Baghdad na kwingineko.
Katika kilele cha utawala wao, mmojawao, Maher Ahmed Mahmoud az-Zubeidi, akifahamika vema kwa jina la utani la Abu Rami, anaaminika kuhusika na mauaji ya watu 200 kila mwezi.
Kama hiyo haitoshi, katili zaidi alikuwa kiongozi mwenzake, Abu Uthman, ambaye alihusika na milipuko katika mapambano mawili mjini Fallujah na kumpatia jina la utani la Abu Nimr likimaanisha Chui.
Majeshi ya Marekani wakamtunuku jina la kichovu zaidi: Number One HVI (high-value individual).
Uthman anahusishwa na mauaji ya mfanyakazi wa kujitolea wa Uingereza, Margaret Hassan na kumteka mwanaharakati wa amani kutoka Uingereza, Norman Kember na kama Rami, amehusika na umwagaji damu wa mamia ya wapiganaji na raia.
Lakini katikati ya 2008, licha ya miaka kadhaa ya kujaribu, vikosi maalumu vya Marekani vilikuwa bado mbali na kusaka ukweli wa watu ambao, kwa kusaidiwa na mtandao mkubwa wa wafuasi, mara chache walilala vitanda hivyohivyo kwa zaidi ya wiki chache.
Warusi pia walikuwa pia wakisawasaka. Rami alikuwa akilaumiwa kwa kuwakata vichwa wafanyakazi wanne wa Ubalozi wa Marekani waliotekwa nyara kutoka kwenye gari lao la kidiplomasia mjini Baghdad na Vladimir Putin akatangaza ofa ya Pauni za Uingereza milioni 7 kwa yeyote atakayefanikiwa kumuua Rami na timu yake nzima mauaji inayomfuata.
Mpaka leo ukubwa wa uwezo wa watu hao wa Al Qaeda haujawekwa hadharani na wala habari za ajabu za jinsi baadaye walivyodhibitiwa.
Gazeti la Mail juzi Jumapili lilifichua kwamba si vikosi maalumu vya Marekani ambavyo mwishowe vilimuua Rami na kumkamata Uthman kama ilivyoripotiwa wakati huo na Gazeti la Washington Post, ila ni SAS.
Waliwezaje kufanya hivyo ilikuwa utendaji bora tulivu ambao mpangokazi ulitumia.
Operesheni zote zilikuwa madhubuti, ngumu kuelezea na zilizopangwa kwa uangalifu, zikitumia ustadi wa hali ya juu.
Huenda zaidi ya yote, ingawa, walikuwa dhahiri wachache kuliko wale wa upande wa Marekani.
Mikakati ilifanyika wakati wa ziara ya miezi sita ya kikosi cha askati cha SAS 'D' mjini Baghdad katika nusu ya pili ya 2008, wakati ambapo milipuko kwenye magari ilishika kasi kwenye mji mkuu huo.
Inafahamika kwamba askari hao walipewa muda kidogo kabla ya kuanza ziara hiyo.
Mamlaka zilizotajwa katika nyaraka zilizopatikana ni pamoja na 'maridhiano ya usalama bila ushahidi wa uhalifu, maridhiano endelevu bila kesi za kutosha za uhalifu, upelekaji katika mifumo ya kisheria bila kesi za kutosha za uhalifu'.
Kwa mujibu wa magazeti, vikosi hivyo vimetumia uhuru mpya kupata mafanikio makubwa, vikikamata mamia ya watuhumiwa wa ugaidi na washirika wao na kuwashikilia katika Vifaa vya Mbinu na Uchunguzi.
Kiuhalisia, uhuru huo ulisaidia kuwezesha uelewa mkubwa wa binadamu uliohitajika kuzuia adui.
Mwaka 2008, Baghdad lilikuwa jiji lililoshikwa na hofu kubwa ya mashambulio ya kigaidi. Waislamu wa Sunni wenye msimamo mkali waliongeza kasi yao ya kutega mabomu kwenye maeneo mbalimbali yaliyokuwa na doria ya hali ya juu katika mji huo.
Lakini muungano uliokuwa ukiongozwa na Uingereza ulikuwa ukijibu mashambulizi, na vikosi maalumu vya Uingereza vilikuwa vikicheza sehemu muhimu.
Hakika, vikosi vya SAS vimemnasa Chui.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item