MAMA ALIYEBAMBWA NA DAWA ZA KULEVYA AELEZA SABABU...

Inaendelea kutoka Jumanne Iliyopita...
Alisema kwamba mtu huyo aliyefahamiana naye siku nyingi kisha akaomba wakutane naye.
"Ni mwerevu mwenye maneno mengi, anaongea sana katika lugha fasaha, lakini unapata kiini cha jambo lenyewe," aliongeza mama huyo.
"Wakati mtu anapokwambia mwanao atakufa, unaelewa kinachomaanishwa.
"Alisema, "Unatakiwa kurekebisha na kurekebisha kuna kazi unatakiwa kufanya." Alinieleza anataka mimi niende Australia na kufuatilia safari za ndege.
"Wiki mbili baadaye alinipigia na kusema itachukua muda kabla ya kunihitaji hivyo akasema natakiwa kurejea India.
"Nilipata pesa zangu baada ya kuuza vito vyangu vya thamani vile vinavyouzwa katika maduka ya Harvey Nicks and Harrods kwa Pauni za Uingereza 800, hivyo nikahitajika kurudi na kupanga shehena."
Mtu huyo kisha akampigia Bibi Sandiford nchini India mapema mwezi Aprili, akimweleza anatakiwa kwenda Bali kumfanyia kazi yake.
"Nilipofika Bali nikawa na mikutano mingi katika migahawa na baa mbalimbali. Ilikuwa ni joho-na-jambia. Mtu huyo angeweza kusema, "Nitakuwa kwenye meza ya tatu mkono wa kushoto. Toa betri kwenye simu yako." Nilidhani ulikuwa upuuzi," amesema.
"Hapohapo aliniambia niende Bangkok na kuishi katika Hoteli ya Amari Atrium kwa siku saba. Alinieleza kuwa mpango mkubwa wa pesa ulikuwa unahusika na kwamba hapo anapata robo yake.
"Ningeweza kupata adhabu ya kifo," alinong'ona, huku aking'ang'ania mikono yangu. "Ninatishwa mno. Ninaweza kufia hapa."
"Nilirudi Bangkok Jumamosi na Jumanne rafiki wa kike wa mtu huyo akarejea. Nilifanya manunuzi naye siku iliyofuata.

"Nilitaka kununua zulia dogo nene kwa ajili ya nyumba yetu ambayo inakaribia kukamilika na yeye alikuwa akitafuta ngozi za wanyama kwa ajili ya viatu na mikoba ya kike.
"Mei 16 alinieleza kwamba kuna mtu atakuja hotelini kwangu siku inayofuata. Alimwita Chubby au kitu kinachofanana na hicho. Alinitumia ujumbe wa maandishi kusema atafika saa 3:00 asubuhi.
"Chubby alipowasili alikuja chumbani kwangu kuchukua begi langu na kwenda nalo sebuleni, kisha akarejea chumbani na kusema, "Begi lako lile pale. Tutaonana Bali." Ni wakati huu ndipo Bibi Sandiford anasema akaamua kutoangalia siri ya kilichomo ndani ya begi lakini badala yake kupakia vitu vyake juu yake.
Hakuna swali kwamba alichokuwa akifanya ni wazi yalikuwa makosa. Na kupigia mstari ukweli, aliamriwa kutupa laini yake ya simu ya mkononi mara tu atakapowasili Bali, kununua nyingine, kuhakikisha kwamba hafuatiliwi na polisi na kujilaza chini kwa siku mbili.
"Niliruka kwa ndege hadi Bali Mei 19 na hapo hapo kuzuiwa. Walijua," amesema Bibi Sandiford.
Maofisa Forodha hapo kabla walisema dawa hizo ziligunduliwa na mbwa maalumu kabla ya begi lake halijafika sehemu ya abiria kuchukulia mizigo.
"Watu wa Forodha walipofungua begi langu hiyo ikiwa ni kwa mara ya kwanza nikaweza kuona kilichomo ndani," alisema. "Hata hapo sikuweza kujua ni nini hasa sababu vilikuwa vimefungwa kabisa. Walinieleza ilikuwa cocaine.
"Nilifikiria kuhusu mfululizo wa matukio kama nikikamatwa? Hapana. Nilifikiria zaidi kuhusu mfululizo wa matukio kama nisingefanya vile.
"Dakika baada ya kukamatwa nikawaza, "Mwanangu amekufa. Nimeshindwa, watamuua mwanangu."
Bibi Sandiford alibaki kimya kwa siku mbili licha, amesema, kuwa amefungwa kwenye kiti. "Kila wakati nilipolala walipiga kelele na kunitaka niamke.
"Niliwapa majina ya uongo na nambari za simu kujaribu kuwalinda wengine lakini baadaye wakaja na kuniwekea bunduki kichwani ndipo nikawaeleza ukweli." Polisi wa Indonesia baadaye wakamshawishi Bibi Sandiford kushiriki kwenye msako mkali kuwanasa wote aliowahusisha.
Alienda kwenye Hoteli ya Puri Nusantara mjini Kuta ambako alichangia chumba na maofisa wawili wa kupambana na dawa za kulevya, na kutuma anuani zake kwa ujumbe wa simu.
"Nilikuwa nimevurugikiwa sababu ya mishipa yangu ya fahamu kuwa kama vile nina homa," alisema.
Bibi Sandiford aliagizwa kutoa kilichomo kwenye begi na kufunika kionekane kama mkebe uliojazwa midoli kwa ajili ya bethdei ya mtoto.
Wakati huo ilikuwa maofisa wawili waliofunika lakini 'wakatengeneza dogo mno'.
Bibi Sandiford amesema, "Niliwaambia watengeneze kubwa na zito kwa sababu ilikuwa kama boksi la karatasi nyepesi. Nilisema, "Hii haiwezi kufanikiwa. Huyu mtu sio mpumbavu, atatazama mara moja na kukimbia." Mipango ya makabidhiano ndipo ikapangwa. "Polisi waliniahidi kwamba wataingilia kati kabla sijaingia kwenye gari," alisema.
"Nilifikiri kama kuna kitu hakitaenda sawa wangeniua au polisi watatoa bunduki zao na kutufyatulia risasi. Nilikuwa nikitetemeka kama jani."
Mawasiliano yakafanyika na Bibi Sandiford akaweka kifurushi kwenye kiti cha mbele.
"Alisema weka kwenye kiti cha nyuma, kisha akaniambia niingie ndani," alisema. "Polisi hawakufanya chochote. Waliniacha niingie ndani ya gari. Mmoja alikuwa kwenye pikipiki mbele kidogo ya barabara.
"Niliambiwa nifungue kifurushi na kuweka kilichomo ndani ya mfuko wa kubebea vinywaji uliokuwa kiti cha nyuma.
"Niliogopeshwa maana sikufahamu polisi waliweka nini ndani. Kam angeona kilichomo hakikuwa alichokuwa akitazamia, angeweza kuniua. Nilikuwa natetemeka sana sikuweza kuchana karatasi. Ndipo polisi walipotusimamisha, wakamhamishia mtu huyo kwenye kiti cha abiria na kuendesha gari mbele zaidi ya barabara hiyo. Wakatupakiza kwenye magari tofauti.
"Niliambiwa, "Funga mdomo wako au utakufa. Kumbuka vijana wako."

"Najua nilichofanya ni makosa lakini ningechagua kufanya kipi? Ningependa kutofanya lakini maisha ya wanangu yalikuwa hatarini.
"Polisi wa kupambana na dawa za kulevya waliahidi watanilinda. Badala yake wamenivalisha suti ya rangi ya machungwa na kunipeleka mbele ya vyombo vya habari kuelezea nikiimba kama ndege.
"Niliwaza, kipi nimefanya?" Nilifanya kumuokoa mwanangu na sasa nimeweka maisha yetu wote hatarini sababu wote tunakabiliwa na adhabu ya kifo. Nimelia sana sijabakiwa na chozi lolote kwa sasa."
Bibi Sandiford, ambaye alikuwa akifanya kazi katika kampuni ya mambo ya sheria ambaye aliwahi kuishi Dubai na Marekani, amesema alifuata mambo makubwa kuwapatia maisha mazuri watoto wake.
Majirani zake wa zamani huko Cheltenham, ambao familia yake ilikuwa ikiishi, mwezi uliopita walimtambua kama "Jirani Kutoka Kuzimu".
Na Bibi Sandiford anakiri: "Ndio tulikuwa hivyo. Nina watoto wawili waliopitia katika mazingira magumu amba wamekuwa wakipigana wenyewe kila wakati.
"Elliot alitakiwa kwenda shule maalumu lakini hawakuwa na nafasi kwa ajili yake kwa miaka miwili. Alikaa nyumbani katika umri wa miaka 12 na 14. Nilikuwa na mtoto mwingine ambaye hajiheshimu, anapigana utadhani kichaa.

Huku akitabasamu alisema: "Nitazame. Naelekea kutumikia maisha yangu yote kwenye kaburi. Nimewezaje kutoka kusikoeleweka hadi katika hili?"

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item