MTOTO ALIYEKUFA AKAA JUU YA JENEZA LAKE NA KUOMBA MAJI...

KUSHOTO: Kelvin Santos. KULIA: Baba wa Kelvin, Antonio Santos.
Mtoto wa kiume wa miaka miwili amekaa juu ya jeneza lake na kuomba maji ya kunywa kabla ya kujilaza tena chali, kwa mujibu wa mtandao wa habari wa Brazili.
Japo hii inaonekana kama ngumu sana kuaminika, moja ya vyanzo vya habari vimedai mtoto Kelvin Santos alisitisha kupumua wakati akipatiwa matibabu ya nimonia katika hospitali moja mjini Belem, kaskazini mwa Brazili.
Alithibitishwa kufa majira ya saa 1:40 usiku Ijumaa na mwili wake ukakabidhiwa kwa familia yake ukiwa umefungwa kwenye mfuko wa plastiki.
Familia ya mtoto huyo huku wakiwa wamechanganyikiwa waliuchukua mwili nyumbani ambako waliwataka ndugu kukesha usiku mzima, huku mwili wa mtoto huyo ukiwa umelazwa ndani ya jeneza lililoachwa wazi.
Lakini saa moja kabla ya mazishi hayachukua nafasi Jumamosi, mtoto ghafla akainuka na kukaa juu ya jeneza lake na kusema: "Baba, naweza kupata majiya kunywa?"
Baba wa mtoto huyo, Antonio Santos alisema: "Kila mmoja akaanza kutetemeka, hatukuamini macho yetu. Kisha tulishani ni muujiza umetokea na mtoto wetu kurudia tena maisha.
"Kisha Kelvin akajilaza tena chali kama alivyokuwa amelazwa mwanzoni. Hatukuweza tena kumwamsha. alikuwa amekufa."
Santos alimkimbiza tena mwanae Hospitali ya Aberlardo Santos mjini Belem, ambako madaktari wakamchunguza tena mtoto huyo na kuthibitisha kwamba hakuonesha dalili za uhai.
Alisema: "Walinihakikishia kwamba hakika alikuwa amefariki. Lakini wakashindwa kunipa ufafanuzi wa kile tulichosikia na kuona nyumbani."
Mwili wa mtoto huyo ukakubalika ucheleweshwe kuzikwa kwa saa nzima kwa imani pengine angeamka tena, lakini hakufanya hivyo hadi alipozikwa majira ya saa 11 jioni ya siku hiyo kwenye makaburi ya watu wa kawaida.
Akishawishika kwamba kifo cha mwanae kimetokana na uzembe wa matibabu, Santos sasa amewasilisha malalamiko yake polisi ambao wameanza kufanya uchunguzi.
Alisema: "Dakika 15 baada ya kumkimbiza hapo tangu alipozinduka, walifika na kuniambia alikuwa amekufa na kunikabidhi mwili wake.
Pengine hawakumpima inavyotakiwa. Mtu aliyekufa hawezi tu kuinuka ghafla na kuanza kuongea. Nimedhamiria kujua ukweli wa hili."
Mamlaka za mji huo zimethibitisha kuwa mtoto huyo alipokelewa hospitalini hapo akiwa katika hali mbaya na kuthibitishwa amekufa baada ya mfumo wake wa upumuaji kushindwa kufanya kazi.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item