MTOTO WA MIAKA MINNE YU MAHUTUTI BAADA YA KUANGUKA DARAJANI...

Binti wa miaka minne yuko mahututi akipigania roho yake baada ya kuanguka kutoka umbali wa futi 30 katika moja ya michezo kwenye hifadhi moja.
Jessica Blake alisemekana kutumbukia kwenye uwazi uliotokana na ubao ulionyofoka kutoka kwenye daraja la kamba na kupelekea kujipigiza kwa kishindo kwenye jiwe katika maonesho ya Chessington World Adventures mjini Surrey.
Binti huyo alipata ufa kwenye fuvu, kuvunjika taya na kutokwa damu kwenye ini na figo zake.
Wazazi wake ambao walitengana, Darren Blake na Sarah Archer wako na binti yao katika Hospitali ya St. George's mjini Tooting, Kusini mwa London. Hali yake inasemekana kuwa mbaya sana.
Shangazi wa Jessica, Carly Hyde anayeishi Watford alisema: "Kulikuwa na kibao kimoja ama viwili vilivyokuwa vikikosekana kwenye daraja. Jessica alikuwa akitembea mbele ya mama yake na ghafla Sarah akaona akitumbukia kupitia kwenye uwazi huo.
"Binti yetu mdogo kwa sasa ni spana mkononi, madaktari wamesema ameumia upande wa kulia wa ubongo wake.
"Kipaumbele chao kwa sasa ni kumweka sawa katika masaa 24 yajayo.
"Wazazi wake hawaivi hata kidogo, yeye ndiye ulimwengu wao wote. Hakika ni malaika mdogo. Familia yote iko kwenye mshituko na kuharibiwa kabisa."
Wiki mbili tu zilizopita Jessica, ambaye alikuwa akiishi na mama yake huko Sheerness, mjini Kent, alisimamia harusi ya baba yake kama binti wadogo walioshika maua mbele ya maharusi.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item