MUUAJI WA TALIBAN ALAZIMISHA KUISHI KWA NGUVU UINGEREZA...
https://roztoday.blogspot.com/2012/06/muuaji-wa-taliban-alazimisha-kuishi-kwa.html
Muislamu wa Afghanistan ambaye amedai kuua watu wakati akiisaidia Taliban ametumia Sheria ya Haki za Binadamu kubakia Uingereza licha ya juhudi za Serikali kutaka kumtimua.
Zareen Ahmadzai, ambaye ametumia miaka mitatau kwenye mapigano Afghanistan, amekiri kutumia bunduki aina ya Kalashnikov na roketi za kutungulia ndege, pamoja na kusambaza silaha na chakula kwa wapiganaji wa Taliban.
Wizara ya Mambo ya Ndani imekataa madai yake ya hifadhi ya kisiasa, na wakati pingamizi lake limetupiliwa mbali, Ahmadzai amekuwa akishikiliwa katika ofisi za uhamiaji za Harmondsworth maalumu kwa ajili ya kuwarejesha makwao wahamiaji zilizoko Magharibi mwa London akisubiria safari.
Bado Zareen mwenye miaka 30 ambaye mwanzoni hakuwa akiongea Kiingereza ameweka pingamizi jipya, aliweza kupindua kesi ya Wizara ya Mambo ya Ndani kwamba maisha yake yatakuwa hatarini endapo atarejea nyumbani.
Uamuzi huo ni msukumo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Theresa May ambaye yuko kwenye shinikizo kufanyania marekebisho ya sheria za haki za binadamu kufuatia mfululizo wa matukio ambapo Waislamu wenye msimamo mkali wamekuwa wakikwepa kurejeshwa makwao.
Ahmadzai aliwasili Uingereza kinyume cha sheria Mei 2010 baada ya kusafiri kutoka Afhganistan kwa kutumia malori.
Siku mbili baadaye alikamatwa kwenye nyumba moja huko Wolverhampton na kudai hifadhi ya kisiasa. Pale Wizara ya Mambo ya Ndani ilipoamuru alirejeshwe kwao, alipinga kwa Mahakama ya Uhamiaji.
Ingawa Jaji alitupilia mbali pingamizi lake, Ahmadzai alipeleka kesi yake kwa Mahakama ya Juu ya Uhamiaji na Hifadhi za Kisiasa.
Baraza la Mahakama lilielezwa Ahmadzai alijiunga na Taliban baada ya baba yake, ambaye alikuwa kamanda kwenye Jimbo la Helmand, kuuawa kwa risasi na askari wa Marekani wakati wa mapambano. Alisema kwamba aliua watu wakati wa mapigano akiwa na Taliban pia alikuwa akisambaza silaha, maji na chakula.
Hukumu ya Mahakama ilisema: "Aliamini alikuwa akitekeleza matakwa ya Uislamu. Alisema baba yake alipigwa risasi wakati wa mapambano la Wamarekani.
"Mrufani alipigana kwa ajili ya Taliban. Alisema kwamba alikuwa akiua watu. Katika matukio tofauti alitumia bunduki aina la Kalashnikov na pia bastola."
Hukumu iliendelea: "Alikuwa akijihusisha na mapigano kwa miaka zaidi ya mitatu kwa mujibu wa mahitaji yake.
"Aliainisha kwamba alikuwa katika mapambano mengi, wakati mwingine mara mbili au tatu usiku na pia mapigano ya wakati wa mchana."
Ahmadzai alidai kwamba wakati alipojaribu kuondoka Taliban baada ya kugundua watu wasio na hatia wanauawa, alikamatwa na kupelekwa mlimani ambako aliteswa sana.
Alidai kwamba kipindi kifupi baadaye alitoroka nchini humo lakini anashindwa kurejea sababu maisha yake yatakuwa hatarini kutoka kwa Taliban na kwa Vikosi vya Ulinzi vya Afghanistan, ambavyo vinapinga Kundi la Waislamu wenye Msimamo Mkali.
Hukumu imesema: "Aliulizwa kwanini asihamie makazi mengine, kwa mfano, kwenda Kabul. Aliulizwa kwa ufasaha endapo wauaji wanatarajia kuhamishia makazi London.
"Alisema polisi watawasaka wauaji kama ilivyo kwa Taliban na mamlaka zitamtafuta pia."
Mtaalamu wa magonjwa ya akili aliyempima Ahmadzai alisema wanaamini alikuwa akisumbuliwa na msongo wa mawazo, ambao unatokana na msongo mkubwa au matukio ya hofu kubwa, kama magwanda ya kijeshi.
Hatahivyo Wizara ya Mambo ya Ndani imepuuza hadithi hiyo ya Ahmadzai na haiamini alikuwa akisakwa na Taliban ama Vikosi vya Usalama vya Afghanista, Jaji Mkuu wa Uhamiaji Jonathan Perkins alihukumu kwamba asirejeshwe. Kesi ilisikilizwa katika mahakama Juni mwaka jana lakini hukumu ikatolewa Machi, mwaka huu.
Msemaji wa Wakala wa Mipakani Uingereza alisema: "Tumesikitishwa sana na uamuzi wa mahakama.
"Hatuamini mtu huyu alihitaji au kustahili ukimbizi katika nchi hii.
"Mara zote tunataka kumuondoa yeyote asiye na haki ya kubaki Uingereza na mwaka jana tumewaondoa zaidi ya watu 52,000."
Wakala haijaafichua kama inajua anakoishi Ahmadzai kwa sasa. Hatahivyo, inafahamika kwamba yuko huru kisheria kuishi kokote katika Uingereza.