MWANAMIELEKA KIJEBA AVUNJIKA MENO YOTE ULINGONI...
https://roztoday.blogspot.com/2012/06/mwanamieleka-kijeba-avunjika-meno-yote.html
Mwanamieleka mbilikimo, Puppet amebamiza chini karibu meno yake yote ya mbele na kukimbizwa chumba cha wagonjwa wa dharura.
Tukio hilo limetokea Jumamosi wakati wa onesho binafsi la "mieleka ya mbilikimo" mjini Virginia ambapo Puppet aliruka na kupita kamba ya juu hadi kwenye meza nje ya ulingo.
Puppet ameeleza aliruka kupitiliza kwa futi kadhaa na badala ya kutua kwenye meza, akajibomeza kwenye sakafu ya saruji…na kujihisi baridi kwa takribani dakika 3.
Imeelezwa alikimbizwa kwenye hospitali ya jirani ya ASAP ambako alishonwa nyuzi 8 kuzipa jeraha juu ya jicho lake. Madaktari walimpatia habari mbaya sana, anahitajika kufanyiwa upasuaji mkubwa kuweka sawa mpangilio wake wa meno yote ya juu.
Kwa sasa Puppet anaendelea kupata nafuu kwa maumivu yaliyotokana na upasuaji, na kama inavyofahamika hatarijiwi kurejea ulingoni katika wiki kadhaa.