WAGUNDUA MZIMU WA MTOTO SEBULENI...


Wapenzi wawili wamedai nyumba yao imevamiwa baada ya kunasa picha za kile wanachoamini kuwa kivuli cha mzimu wa mtoto kwenye kamera.
Akiwa mwenye hofu, John Gore mwenye miaka 43 alikuwa akichua picha za paka wake pale alipogundua mchoro wa umbo la mzimu mdogo.
Umbo hilo ambalo linaonekana kama mtoto anayetambaa, inaonekana kusimama kando ya kiti kwenye sebule ya nyumba ya John anayoishi na rafiki yake wa kiume, Sonia Jones huko Cheltenham, Gloucestershire.
Wapenzi hao kwa sasa wameupachika jina mzimu huo, Johnny Junior'.
Majirani waliwaeleza wapenzi hao hapo kabla kwamba mtoto huyo alifariki kwenye kifanda kidogo cha safari nyumbani kwao miaka kadhaa iliyopita.
John na Sonia wamegundua pia taa cha chumbani humo huwaka na kuzima na televisheni kubadilisha chaneli yenyewe katika mfululizo wa matukio ya kipepo katika nyumba hiyo.
John alisema: "Mmoja wa paka wangu alikuwa akikwangua ukutani na kuruka juu eneo hilo na mara zote tulikuwa tukichukua picha za paka hao.
"Pale tulipotazama kwa makini tulishangaa kuona umbo la mtoto aliyesimama kando ya sofa.
"Ni kitu kipya mno ambacho hakijawahi kutokea hapo kabla, kama televisheni kuendelea kujibadilisha chaneli na kujizima yenyewe.
"Nilionesha picha hiyo kwa binti mmoja barabarani ambaye aliishi hapa kwa miaka. Aliniambia mtu mmoja aliyekuwa akiishi katika nyumba hii kabla yetu alikuwa na mtoto aliyefia kitandani."
Lakini wapenzi hao hawana mipango yoyote ya kuondoka na wameupachika mzimu huo jina la utani la 'Johnny Junior' na kuamini kuwa ni mzimu rafiki.
John alisema: "Najisikia vizuri kuhusu hili na pia Sonia, haitusumbui sababu ni mzimu ambao ni rafiki.
Nilianza kuamini mizimu baada ya mama yangu Anne kufariki mwaka 2004, lakini watu kila mara wanasema mpaka utakapoona ndipo utaamini.
"Ni ngumu kuelezea kama ni mvulana au msichana, lakini tumeuita mzimu huo Johnny Junior, na unaonekana kuwa katika rika la mtoto anayetambaa.
"Watu wengi wameuona na wanatoa maoni yao katika mtandao wa Facebook. Wengine wamesema unaonekana kama kivuli, lakini ni picha kamili ya umbo la binadamu."

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item