ASKARI WA JWTZ WALIOKUTWA NA MBAO ZA WIZI WAPANDA KIZIMBANI...

Watu tisa wakiwamo askari wawili wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliokamatwa wiki iliyopita wakiwa na mazao ya misitu ndani ya Pori la Akiba la Kigosi, wamefikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa mjini hapa kujibu mashitaka mawili kila mmoja.
Katika kesi ya kwanza inayokabili watu watatu, Koplo Moshi Jumanne, Koplo Mustafa Yusuph na Sophia Shigemela, ilidaiwa mbele ya Hakimu Mkazi, Hamis Bally jana kuwa walitenda makosa hayo Septemba 7 katika kijiji cha Mnange, Kaliua.
Upande wa mashitaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali Rwegire Deusdedit, ulidai kwamba siku hiyo usiku, washitakiwa walikutwa wakimiliki kinyume cha sheria mbao 633 mali ya Serikali bila kuwa na kibali au leseni.
Wakili Rwegire alidai katika mashitaka ya pili, kwamba siku hiyo, washitakiwa walikamatwa wakisafirisha mbazo hizo zenye thamani ya Sh 6,330,000 kwa kutumia gari ambalo ni mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kibali.
Washitakiwa wote watatu walikana mashitaka na wako nje kwa dhamana ya mtu mmoja ya Sh milioni moja kila mmoja kwa kiasi hicho hicho. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Oktoba 8 kwa kuwa upelelezi haujakamilika.
Katika kesi ya pili dhidi ya watu sita, Richard Samwel, Gasper Kagutwa, Sultan Hadan, Mashiba Lugaka, Msina John na Kiwele William, ilidaiwa kuwa washitakiwa walitenda makosa yao Septemba 7, katika kijiji cha Mwendakulima, Kaliua.
Wakili wa Serikali, Rwegire Deusdedit alidai mbele ya Hakimu Bally kuwa siku hiyo watuhumiwa hao walikutwa wakimiliki mbao 422 kinyume cha sheria.
Akiwasomea mashitaka ya pili, Wakili alidai siku hiyo washitakiwa walikutwa wakisafirisha mazao hayo yenye thamani ya Sh 4,220,000 kwa gari aina ya Fusso namba T761 BCV.
Washitakiwa wote walikana mashitaka yao na Mahakama ilitaka walete wadhamini wawili kila mmoja kwa ahadi ya Sh milioni mbili. Kesi iliahirishwa hadi Septemba 24 itakapotajwa tena.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item