CHEKA TARATIBU...

Mchina anashindana na Mswahili kunywa bia kwenye baa moja katikati ya jiji la Dar es Salaam. Kila akinywa bia tano, yule Mchina anapiga pushapu na kuingia chini ya meza kisha anatokea upande wa pili na kuendelea hadi akafikisha kreti tano huku akionekana hana dalili za kulewa. Mswahili kuona anaelekea kushindwa huku akiwa tayari kaanza kulewa, akaamua naye kuiga mbinu za yule Mchina. Naye akaamua kusogea kando na kupiga pushapu. La haula! Kuchungulia chini ya meza akaona kuna Wachina kumi wamebanisha uvunguni. Duh...

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item