KIJANA ACHOMWA KISU NA KUFA AKIAMULIA UGOMVI...

KUSHOTO: Chupa za pombe bado ziliendelea kuwapo eneo la sherehe. KATI: Polisi wakiendelea kuchunguza eneo la tukio. KULIA: Jay Whiston.
Mwanafunzi mpole na mkarimu alichomwa visu na kufa akijaribu kumlinda rafiki yake baada ya vijana kuzamia kwenye sherehe waliyoiona kupitia mtandao wa Facebook.
Jay Whiston mwenye miaka 17, alichomwa kisu tumboni nje ya nyumba ya mwandaaji wa sherehe hiyo wakati akijaribu kuwazuia wahalifu hao wasimwibie rafiki yake simu yake ya mkononi.
Ghasia zililipuka pale vijana ambao hawakualikwa walipovamia nyumba hiyo kwenye nyumba za makazi katika barabara inayoelekea sokoni na kuanza kuwabughudhi wageni.
Jay alishambuliwa wakati akijaribu kumsaidia rafiki yake.
Mzozo huo ulianzia kwenye bustani kabla ya kusambaa mtaa mzima.
Gari la wagonjwa liliitwa eneo la tukio lakini kijana huyo ambaye alikuwa akisomea sheria, biashara na teknohama kwenye Chuo cha Teknolojia cha Tendring na kutabiriwa kupata daraja A, alifia hospitalini.
Mama yake, Caroline Shearer mwenye miaka 47, juzi alisema kwamba Jay hakuwa akipendelea kupigana na ugomvi na jaribio lake kujaribu kuepusha mapigano ndivyo has alivyo.
"Alikuwa akijaribu kumlinda mmoja wa rafiki zake ambaye alikuwa akizongwa na jamaa kadhaa kwamba alikuwa kazamia sherehe na walikuwa wakijaribu kuchukua simu za mikononi za watu," alisema.
"Jay alikwenda pale na kuwataka wamwachie."
Aliongeza, "Alikuwa mpole kabisa ambaye alikuwa mkarimu na hakuwa na maadui."
"Hii ni ndoto mbaya kabisa kwa kila mama. alipendwa na kila mmoja na alikuwa mwenye kujali sana.
"Mwanangu hakuwahi kuwa na matatizo na polisi kabla. Alichukia mapigano na alichukia watu wasiotenda haki.
"Bado najisikia ganzi lakini naanza kuhisi hasira sasa. Kwa vipi wahuni wapoteze maisha yasiyo na hatia jinsi watakavyo? Hakuna sababu ya kufanya hivyo.
Alikuwa na mipango katika maisha yake. Alitaka kumiliki nyumba yake mwenyewe, kuwa mweka rehani kama baba yake na kufunga ndoa na kuwa na watoto wa kike wawili. Sasa hatutaweza kushuhudia hayo yakitokea."
Wazazi wa mwandaaji walikuwa kwenye nyumba hiyo ya vyumba vinne vya kulala yenye thamani ya Pauni za Uingereza 450,000 iliyoko Colchester kusimamia sherehe hiyo lakini watu 200 wakazamia na kufanya idadi ya waalikwa kuwa mara mbili zaidi ya ilivyotarajiwa, baada ya taarifa kuzagaa kwenye mitandao ya Facebook na Twitter.
Mamia ya meseji yalisambazwa kwenye Twitter masaa kadhaa kabla ya mauaji, ikiwamo moja iliyosema, "Sherehe kubwa sana mjini Stanway, yeyote ruksa kuhudhuria."
Nyingine ilisema: "Jamaa fulani wana sherehe huko Stanway na wanawaalika wote mjini Colch!" Meseji zaidi zilisomeka: "Imetangazwa kote katika Twitter na fb (Facebook)."
Watu wanne, wawili wanaume wenye miaka 18 na wawili wavulana wa miaka 17, wote kutoka Colchester wanashikiliwa na polisi kuhusiana na mauaji hayo.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item