MWILI WA ALIYEZAMIA KWENYE NDEGE WADONDOKA MTAANI...
https://roztoday.blogspot.com/2012/09/mwili-wa-aliyezamia-kwenye-ndege.html
Polisi wakiufunga vizuri mwili wa mzamiaji huyo tayari kwa kwenda kuuhifadhi. PICHA NDOGO: Wahusika wakifanya usafi sehemu ulipodondoka mwili wa mzamiaji huyo.
Mzamiaji amedondoka umbali wa maelfu ya futi kutoka katika ndege kwenye mtaa wa kitongoji kimoja tulivu baada ya kuwa amejificha kwenye magurudumu ya ndege hiyo.Mwili wa mtuhumiwa huyo, ambaye anakadiriwa kuwa na miaka 30 hivi na anayetokea Kaskazini mwa Afrika, uligunduliwa katika kijito kilicho jirani na jiji la London kando ya njia zinapotua na kuruka ndege.
Wataalamu wa masuala ya ndege wamesema anawezekana kuwa alishakufa hata ya kujibamiza chini ama sababu aligandamizwa na gurudumu muda mfupi baada ya ndege kuruka au sababu ya baridi kali katika uwanda wa juu kutoka usawa wa bahari.
Inadhaniwa kuwa mwili wa mwanaume huyo ulidondoka kutoka kwenye ndege hiyo wakati ndege hiyo ikitoa magurudumu yake katika harakati za kutua.
Wakazi wa barabara yenye miti iliyopangana mstari huko Mortlake, kusini kabisa mwa Thames pungufu ya maili 10 kutoka uwanja wa ndege, jana waliongelea mshituko wao kukuta mwili huo baada ya kusikia kishindo kikubwa.
Billy Watson mwenye miaka 26, mlinzi anayeishi mkabala na eneo ulipodondoka mwili wa mtu huyo, alisema aliona mwili huo 'ukielea hewani'.
Alisema: "Huwezi kuamini. Kitu cha kwanza kufikiri nilipoona mwili huo kilikuwa kwa,ba lazima umeanguka kutoka umbali mrefu kidogo.
"Ungeweza kueleza mwili wake uliraruliwa. Kulikuwa na dimbwi kubwa sana la damu kichwani mwake."
Juzi usiku, wengine walisema wameshangazwa damu kuendelea kuonekana kwenye mitaa yao. Catherine Lambert, mama wa watoto wawili, alisema 'ilikuwa inakera' kwamba eneo la tukio halikusafishwa.
"Inashitusha unaweza kuendelea kuona mabaki ya damu," alisema, akaongeza kwamba mwili huo ulitelekezwa bila kufunikwa na polisi kwa 'masaa kadhaa' tangu ulipogundulika.
Alisema: "Tunashangaa nini kilimfanya aingie kwenye ndege ile na kutaka kujificha." Mkazi mwingine, ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema: "Hakuna aliyemuona wakati akianguka maana ilikuwa mapema sana asubuhi siku ya Jumapili.
"Kwa namna yoyote alivyokuwa akitaka kujificha lazima ilikuwa inaogopesha sana kwake kufanya vile."
Richard Taylor, kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga, alisema wazamiaji wanaojificha kwenye magurudumu ya ndege wana nafasi finyu mno ya kupona kutokana na ama kupondwa na magurudumu baada ya kuruka au kuganda kwenye baridi kali inayofikia nyuzijoto -40.
Alisema: "Nafasi za kuishi kwa mzamiaji ni finyu sana, hasa wanaobana kwenye magurudumu.
Wakati magurudumu yanapotoka nje upande mwingine, maili chache kutoka njia ya kuruka na kutua, na takribani futi 2,000 angani, kama kuna mtu aliyekufa lazima atadondoka."
Polisi walisema walikuwa wakichunguza endapo mwili huo ulikuwa wa mzamiaji."
Ugunduzi huo umekuja wiki mbili tu baada ya mwili wa mzamiaji kukutwa kwenye magurudumu ya ndege ya British Airways iliyokuwa ikiwasili katika Uwanja wa Heathrow kutokea Cape Town, Afrika Kusini.
