YABAINIKA SILAHA MOJA ILITUMIKA KUANGAMIZA FAMILIA...
https://roztoday.blogspot.com/2012/09/yabainika-silaha-moja-ilitumika.html
Silaha moja ilitumika kufanya mauaji ya Alpine ambapo watu wanne wakiwamo wanandoa wa Kiingereza walipigwa risasi na kufa, imefahamika.
Ugunduzi usio wa kawaida umeongezea nguvu nadharia kwamba mauaji hayo yalifanywa na muuaji wa kukodi aliyepata mafunzo ya hali ya juu kabisa.
Hii imefahamika baada ya binti wa miaka saba ambaye alinusurika katika shambulio hilo kuongea na polisi wa Ufaransa kwa mara ya kwanza baada ya kutoka kwenye chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu alikolazwa akiwa mahututi.
Uchambuzi wa kina wa mwendo wa risasi wa maganda 25 yaliyotumika na kukutwa eneo la tukio karibu na Ziwa Annecy, mashariki mwa Ufaransa, umeonesha zote zimetoka kwenye bastola moja maalumu yenye kipenyo cha milimita 7.65.
Zote zilitumika kuwaua Saad Al-Hilli mwenye miaka 50, mkewe Ikbal mwenye miaka 47, mama yake Suhaila Al-Allaf mwenye miaka 74, na Sylvain Mollier mwendesha baiskeli wa Ufaransa mwenye miaka 45.
Msaliaji Zainab al-Hilli, alijeruhiwa vibaya maeneo mbalimbali mwilini baada ya kupigwa risasi na kushambuliwa wakati wa shambulio hilo na kulazimisha madaktari kumweka katika chumba cha mahututi.
Hatimaye baadaye akaanza kupata nafuu na kuweza kufanya mahojiano mafupi na maofisa wa polisi nchini Ufaransa, vyanzo vya habari vilivyo karibu na uchunguzi vimesema.
Alionekana kama shahidi muhimu katika shambulio hilo la kutisha ambalo lilichukua uhai wa wazazi wake pamoja na bibi yake.
Mdogo wa Zainab, Zeena mwenye miaka minne, ambaye alinusurika baada ya kujificha nyuma ya mama yake, amesafirishwa kwa ndege kurejea Uingereza na waangalizi.
Licha ya kushindwa kutoa mwanga zaidi kuhusu wauaji hao, Polisi wa Ufaransa wanaamini Zainab anaweza kuwapa taarifa muhimu kuweza kujua hasa nini kilichotokea.
Chanzo cha habari kilisema: "Wameweza kuongea naye lakini huu ulikuwa ni mkutano wa kuanzia tu. Hawawezi kuongelea kwa kina zaidi na mtoto huyo alikuwa amechoka mno. Haikuruhusiwa mahojiano hayo kuendelea zaidi."
Polisi sasa watalazimika kusubiri ruhusa kutoka kwa madaktari kabla ya kumhusisha binti huyo katika mahojiano yoyote marefu pale atakapotarajiwa kuulizwa anachokumbuka kuhusu shambulio lile.
Haijafahamika mara moja nani atakayewatunza watoto wawili hao yatima kwa sasa.
Juzi asubuhi, kikosi cha mabomu kilikagua nyumba ya familia baada ya polisi kubaini vitu 'vilivyohusika'.
Polisi walifunga barabara zote zinazozunguka nyumba hiyo huko Claygate, Surrey, na kuhamisha majirani wakati ugunduzi wa vitu kadhaa visivyo vya kawaida ukiendelea.
Plastiki ngumu ilisimamishwa nje ya mlango wa mbele wa Al-Hilli na uchunguzi umeelezwa kulenga vitu vilivyogunduliwa kwenye mabaki ya mali.
Msemaji wa polisi wa Surrey alisema kwamba vizuizi vimepanuliwa zaidi.
Walisema: ""Polisi wa Surrey wanaweza kuthibitisha kwamba kutokana na mazingira ya vitu vilivyogundulika eneo hilo huko Oaken Lane, Claygate, maofisa wa polisi wamepanua vizuizi kuzunguka nyumba hiyo.
"Majirani katika maeneo ya jirani wamehamishwa kwa muda."
Msemaji huyo baadaye alisema kwamba hakuna kitu chochote cha hatari kilichogundulika katika nyumba hiyo na watu wanaweza kwenda makwao.
Balsam Hilli-Xanthis mwenye miaka 59, binamu wa mzaliwa wa Irak, Al-Hilli, amejitolea kuwasaidia kifedha watoto hao yatima.
Chanzo cha habari kutoka familia hiyo kilisema: "Balsam aliwapigia simu polisi wa Surrey. Alisema yuko Irak kwa sasa. Hakutuma maombi rasmi ya kuwatunza, alisema anatoa msaada, hasa wa kifedha."