ALIYEJERUHI KWA RISASI, NAYE SASA AUAWA KWA RISASI...
https://roztoday.blogspot.com/2012/12/aliyejeruhi-kwa-risasi-naye-sasa-auawa.html
![]() |
| KUSHOTO: Eneo ambapo Jamie Starkey alipigwa risasi na kufa. KULIA: Jamie Starkey. |
Kijana ambaye alimpiga risasi mhusika wa dawa za kulevya ili kumzuia asiishambulie familia yake ameuawa kwa risasi na muuaji wa kulipwa wiki chache tu baada ya kuachiwa kutoka jela.
Jamie Starkey alikuwa na miaka 16 tu wakati alipompiga risasi na kumjeruhi Daniel Gee majira ya saa 11 alfajiri ya Siku ya Mwaka Mpya nje ya baa.
Alitumikia kifungo cha miaka mitatu na nusu jela katika kifungo cha miaka saba kabla ya kuachiliwa mapema mwaka huu.
Saa 2 usiku wa Jumapili Starkey, ambaye sasa ana miaka 21, alikuwa akitembea kuelekea kwenye gari lake nje ya nyumba yake huko Fazakerley, mjini Liverpool, ndipo muuaji aliyevalia nguo nyeusi alipomtandika risasi.
Muuaji huyo alikimbia akikatisha uwanja wa mazoezi na akumwacha Starkey akikata roho.
Juzi, Polisi wa Merseyside walitarajiwa kumhoji Gee ambaye ana umri wa miaka 33, gerezani ambako anatumikia kifungo kwa kosa la kutishia kumuua Starkey katika shambulio la kulipiza kisasi.
Polisi hapo kabla walirekodi kwa siri majibizano ambapo Gee alisema: "Usiwe na shaka dogo mpumbavu anakwenda ... sehemu pekee aliyo salama ni jela na hawezi kuwa salama huko ... inawezekana kuwa pabaya zaidi huko ... kuliko kuwa nje. Nitamchinja koo lake."
Msemaji Mkuu wa polisi wa Merseyside, Jon Ward alisema: "Haya ni mauaji ya kikatili, ufyatuaji risasi wa kimahesabu kwa kijana wa miaka 21 ambaye hivi karibuni aliachiwa kutoka gerezani baada ya kumpiga risasi mwanaume mwingine katika Siku ya Mwaka Mpya 2008.
"Hakuna shaka kwamba hili lilikuwa shambulio la kudhamiria na kwamba yeyote aliyefanya hivi alikusudia kumuua Starkey.
"Tunaamini kwamba baadhi ya wafuasi wa jamii ya watu wenye hali moja watajua nani aliyefanya hivi na watajua nani aliye nyuma yake na ninawaomba kuwasiliana nasi.
"Jamie Starkey alikuwa na miaka 21 tu na alikuwa na malengo yake kwa maisha ya baadaye, lakini alichagua njia ambayo kwa haraka ikampeleka kwenye mauti yake.
"Polisi wa Merseyside wanawajibika kupambana na mashambulizi ya bunduki na kuwakamata watuhumiwa mitaani na ninaweza kuwahakikishia tena wananchi wa kawaida kwamba tunafanya kila lilalowezekana ndani ya uwezo wetu kuwasaka wahusika wote wa mauaji haya ya risasi.
"Doria zimeongezwa katika eneo hilo kuweka uhakika na eneo la tukio la mauaji hayo limefungwa ili kupisha uchunguzi wa kina kuweza kufanyika.
"Uchunguzi wa kina na mapana unafanyika na ningeomba kwa yeyote aliyeshuhudia tukio hilo, au yeyote aliyeona mtu mwenye mashaka kwenye eneo la tukio masaa kadhaa kabla ya mauaji hayo kuja kutupa taarifa."
Mwaka 2008 Mahakama Kuu ya Liverpool ilielezwa kwamba Starkey, ambaye alikuwa akipitia kipindi kigumu, alimfyatulia risasi Gee baada ya kudai familia yake ilikuwa akihangaika kwa miezi kadhaa ya vurugu na vitisho.
Gee alisemekana kurandaranda akiwa ndani ya gari lake aina ya Range Rover lenye thamani ya Pauni za Uingereza 60,000 akiwapigia mluzi watoto aliowaajiri kusambaza dawa za kulevya kwa kutumia baiskeli.
Wanasheria wa Starkey walidai genge la Gee lilitupia matofali kwenye nyumba ya familia ya Starkey, kuharibu gari la kak yake na kuwatisha mara kwa mara ndugu zake.
Katika tukio moja washirika wa Gee walisemekana kuvunja kila dirisha nyumbani kwa Starkey na kumkata kwa vioo mdogo wake wa kike mwenye miaka minne.
Kisha siku chache kabla ya Gee kupigwa risasi inadaiwa mhusika huyo wa dawa za kulevya alimteka nyara mmoja wa marafiki wa Starkey na kumfungia kwenye nyumba moja iliyotelekezwa ambako alimponda kwa mawe.
Katika sherehe ya Mwaka Mpya, Starkey alitoka kusherehekea mjini Everton ambako alikutana na mmoja wa marafiki wa Gee ambaye alimtishia kumpiga risasi. Kijana huyo alikimbilia kwenye nyumba iliyotelekezwa ng'ambo ya barabara ambako bastola aina ya Colt ilikuwa imefichwa.
Katika kipindi cha dakika 15 za makabiliano nje ya baa majira ya Saa 11 alfajiri ya siku iliyofuata, mashuhuda walisikia Gee akitoa vitisho kwa familia ya Starkey na kumchochea. Wakati fulani, Gee alimweleza: "Nifyatulie risasi sasa au nakwenda kumuua mama yako."
Starkey akafyatua risasi na moja ya risasi ikampiga Gee tumboni, kumchana pafu, na kwenda moja kwa moja mgongoni mwake. Alipelekwa hospitali lakini akakataliwa kupatiwa matibabu.
Siku nne baadaye Gee alikamatwa kwa kusambaza dawa za kulevya katikati ya jiji na akahukumiwa miaka saba na nusu jela, Juni 2008.
Starkey alihukumiwa kifungo jela Oktoba 2008 baada ya kukiri kujeruhi kwa kukusudia na kumiliki silaha ya moto kwa lengo la kutishia maisha.
Ilibainika kufuatia kupigwa risasi kwa Gee, ambaye alimtumia Starkey ujumbe wa maandishi akimuahidi kumpatia Pauni za Uingereza 20,000 ili asizungumze na polisi wa zamu, alipanga kulipa kisasi ndani ya masaa tangu kujeruhiwa kwake.
Polisi walipokwenda kuongea naye kuhusu kujeruhiwa kwake Gee alisema: "Msijali nitamkamata huyo panya mdogo."
"Hakuna ubishi kwamba hili ni shambulio lililokusudiwa na yeyote aliyehusika alidhamiria kumuua Jamie Starkey."