CHEKA TARATIBU...
https://roztoday.blogspot.com/2012/12/cheka-taratibu_4.html
Wanafunzi walipewa zoezi la kuchora jiwe likianguka kutoka mlimani. Wakati akipitia kazi hizo za wanafunzi wake, mwalimu akagundua karatasi moja iliyoandikwa jina tu bila picha yoyote. Akamwita yule mwanafunzi na kuhoji kulikoni? Mwanafunzi akajibu, "Nilipomaliza tu kuandika jina, nikashitukia jiwe limetua kichwani nikapoteza fahamu!" Balaa...
