DAKTARI NA MUUGUZI MOI KORTINI KWA KUOMBA RUSHWA MGONJWA...
https://roztoday.blogspot.com/2012/12/daktari-na-muuguzi-moi-kortini-kwa.html
Daktari na muuguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaa, wakikabiliwa na mashitaka ya kuomba na kupokea rushwa ya Sh 1.5.
Washitakiwa wakiwa wafanyakazi wa hospitali hiyo Kitengo cha Mifupa (MOI), walidaiwa kujipatia fedha hizo kutoka kwa ndugu wa mgonjwa ili waharakishe kumfanyia operesheni ndugu yake.
Washitakiwa hao, Dk Deodatha Maziko (30) na Erick Kimwomwe (28) ambaye ni muuguzi, walisomewa mashitaka na Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Allen Kasalama mbele ya Hakimu Hellen Liwa.
Wakili Kasalama alidai kuwa Novemba 27, mwaka huu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Kitengo cha Moi, washitakiwa waliomba rushwa ya Sh milioni 1.5 kutoka kwa Stanford Mhina ili ndugu yake Fanueli Mhina afanyiwe oparesheni.
Fanueli alikuwa amelazwa katika wodi namba 18 ya Sewa Haji akisubiri kufanyiwa operesheni.
Wakili wa Takukuru aliendelea kudai katika mashitaka mengine kuwa Novemba 29, mwaka huu katika hospitali hiyo, washitakiwa walipokea Sh milioni moja kutoka kwa Mhina kama kishawishi cha kuharakisha operesheni ya Fanueli jambo ambalo ni kinyume cha maadili yao ya kazi.
Washitakiwa walikana mashitaka na kutakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaofanya kazi serikalini watakaosaini hati ya Sh milioni 1.5 kila mmoja na washitakiwa wawasilishe hati zao za kusafiria.
Dk Maziko alipata dhamana na Kimwomwe alirudishwa ruamande kwa kutotimiza masharti ya dhamana na upelelezi haujakamilika. Kesi itatajwa tena Desemba 20, mwaka huu.