DENI LA DOWANS TANESCO BALAA, SASA LAFIKIA SHILINGI BILIONI 122...
https://roztoday.blogspot.com/2012/12/deni-la-dowans-tanesco-balaa-sasa.html
![]() |
| Mitambo ya iliyokuwa Dowans eneo la Ubungo, Dar es Salaam. |
Deni la Kampuni ya Kufua Umeme ya Dowans kwa Shirika la Umeme (Tanesco) limefikia zaidi ya Sh bilioni 122 kutokana na kuongezeka kwa riba ya asilimia 7.5 ya deni la awali kila siku.
Hali hiyo imeendelea kuilemea Tanesco wakati Mahakama ya Rufaa Kanda ya Dar es Salaam jana ikishindwa kusikiliza rufaa iliyokatwa na Tanesco, kupinga kulipa deni hilo.
Wakili wa Dowans, Kennedy Fungamtama alidai jana kuwa hadi kufikia Novemba 20, mwaka huu, deni la Dowans kwa Tanesco lilifikia Dola za Marekani milioni 76.3 sawa Sh bilioni 122.
Kabla ya riba hiyo inayotozwa kila siku, Tanesco iliamriwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC), kuilipa Dowans Sh bilioni 96 kutokana na kuvunja mkataba kinyume cha sheria.
Jana rufaa ya kesi hiyo ilitakiwa kuanza kusikilizwa, hata hivyo, kiongozi wa jopo la majaji linalosikiliza rufaa hiyo, Jaji Bernard Luanda aliahirisha kesi hiyo kwa kuwa Jaji Catherine Oriyo ambaye yupo kwenye jopo hilo, alitoa uamuzi katika kesi moja iliyohusu Dowans na Tanesco iliyokatiwa rufaa.
Jaji Oriyo alisikiliza na kutoa uamuzi katika kesi ilifunguliwa katika Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara ambayo Dowans waliiomba mahakama hiyo kupitia upya hukumu hiyo.
Katika maombi yaliyowasilishwa na Tanesco, waliomba zuio la utekelezaji wa malipo ya Sh bilioni 96 kwa Kampuni ya Dowans iliyotolewa na ICC kama ilivyoamuliwa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Hata hivyo, Tanesco iliamuriwa kulipa fedha hizo kutokana na kuvunja mkataba wa biashara na Dowans kinyume cha sheria na Mahakama ya ICC kuwataka walipe fedha hizo baada ya kusajili tuzo ya malipo katika Mahakama Kuu. Hata hivyo, Tanesco ilipeleka taarifa ya kusudio la kutaka kukata rufaa.
Dowans nao waliiomba Mahakama kutupilia mbali taarifa ya Tanesco ya kusudio la kukata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa katika Mahakama Kuu iliyokubali usajili wa tuzo ya Dowans na kuwataka Tanesco kulipa fedha hizo.
Maombi hayo awali yalipangwa kusikilizwa mbele ya jopo la majaji watatu akiwamo Jaji Luanda, Jaji Natalia Kimaro na Jaji Oriyo. Hata hivyo, Jaji Luanda jana alisema watatoa tarehe ya kusikilizwa kwa maombi hayo baada ya kupangwa kwa jopo jipya.