IMETIMIA MIAKA 20 TANGU KUTUMWA MESEJI YA KWANZA YA SIMU YA MKONONI...
https://roztoday.blogspot.com/2012/12/imetimia-miaka-20-tangu-kutumwa-meseji.html
Jana ilikuwa ni maadhimisho ya miaka 20 tangu kutumwa meseji ya kwanza ya maandishi. Ilikuwa Desemba 3, 1992, ambapo Mhandisi Neil Papworth anayefanya kazi nchini Uingereza alituma ujumbe wa kwanza mfupi wa maandishi (SMS) uliosomeka "Merry Christmas" (Heri ya Krismasi).
Hatahivyo, Papworth alikuwa peke yake wakati alipobofya kitufe cha kutuma katika meseji hiyo ya kwanza. Akiwa na umri wa miaka 22, Papworth alikuwa akifanya kazi katika kampuni inayoitwa Semea Group Telecoms, ambayo ilikuwa ikijihusisha na mradi wa meseji za simu za mikononi kwa ajili ya Vodafone, wakala wa simu za mikononi Ulaya.
"Ilitokea siku hiyo kwamba Vodafone walitaka kujaribu kutuma meseji kwa Richard Jarvis, mmoja wa wakurugenzi pale, ambaye alikuwa katika sherehe ya Krismasi. Hivyo tulikaa kwenye kompyuta na kumwandikia meseji na kisha kumtumia ujumbe wa 'Merry Christmas," Papworth aliliambia shirika la habari la ABC. "Kwangu mimi ilikuwa siku nyingine ya majaribio, haikuonekana litakuwa jambo kubwa kwa wakati huo."
Lakini, likabadilika kuwa kitu kikubwa mno. Katika siku hiyo mwaka 1992, Papworth hakutuma meseji yake ya kwanza kwa kidole chake katika simu ya mkononi. Alituma kutoka kwenye kompyuta kubwa katika moja ya ofisi za Vodafone kwenda kwenye simu ya mkononi aina ya Orbatel 901, ambayo ilikuwa na ukubwa wa simu za ofisini za wakati huu, anafafanua Papworth.
Papworth sio kwamba ndiye mvumbuzi wa meseji za maandishi bali asili yake ni wazo la mwaka 1984 kutoka kwa Matti Makkonen, Mhandisi wa Finland, aliyekuwa akifanya kazi na Nokia katika utumaji meseji wa simu za mikononi.
Wakati huo, uliweza tu kupokea meseji kwenye simu; hukuweza kutuma ujumbe kutoka kwenye simu hadi baada ya mwaka au zaidi pale simu kutoka Nokia na wengineo walipokuwa na uwezo unaostahili.
"Miaka ilisonga mbele na watu wakaweza kuanza kutuma meseji za maandishi. Ilichukua miaka michache kuweza kufanikiwa," alisema Papworth. "Lakini ilipoadhimishwa miaka 10 ilikuwa imesambaa vya kutosha kwa wakati huo."

Wow, thiѕ аrticle is fastіdious, my ѕisteг is
ReplyDeleteanаlyzing suсh things, thеrefοre I am going
tο let know her. http://www.tlcsavings.сo.uk
Have a look at my web site : new phone line