AHUKUMIWA VIBOKO 6 KWA KUMDUNGA MIMBA MWANAFUNZI...

Mkulima mkazi wa Itega katika Manispaa ya Dodoma,  Mahamoud Athumani (17), amehukumiwa adhabu ya kuchapwa viboko sita baada ya kupatikana na hatia ya kumpa mimba mwanafunzi wa Kidato cha Tatu wa Shule ya Sekondari Itega.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma,  Elinaza Luvanda.
Akitoa hukumu hiyo Hakimu Luvanda alisema kuwa ameridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka na akamhukumu mshtakiwa adhabu ya kuchapwa viboko.
Hata hivyo alipotakiwa kutoa utetezi wake, mshitakiwa alisema kuwa hana lolote la kuzungumza na kuomba Mahakama imtetee.
Hakimu Luvanda alisema kuwa hukumu hiyo imezingatia umri wa mshtakiwa ambao ni miaka 17.
Awali, Wakili wa Serikali Mwandamizi  Godfrey Wambali aliiomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa kutokana na kosa alilolifanya.
Kulingana na hati ya mashitaka, siku isiyojulikana mwezi Desemba mwaka 2011, katika Kijiji cha Itega, Manispaa ya Dodoma Mkoa wa Dodoma, mshitakiwa alimpa mimba binti wa miaka 18 ambaye alikuwa mwanafunzi wa Kidato cha Tatu Shule ya Sekondari Itega.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item