ATENGENEZA SHATI LA DHAHABU KUWANASA WASICHANA...
https://roztoday.blogspot.com/2013/01/atengeneza-shati-la-dhahabu-kuwanasa.html
Datta Phuge. |
Imekuwa ikielezwa mara kwa mara kwamba pesa haiwezi kununua mapenzi.
Lakini inajaribu kueleza hivyo kwa tajiri wa Kihindi ambaye ambaye ametumia Pauni za Uingereza 14,000 kwa ajili ya shati gumu la dhahabu kwa matumaini kwamba litamsaidia kuwanasa wasichana.
Kimwaga huyo Datta Phuge mwenye miaka 32 kutoka Pimpri-Chinchwad, amegharamia shati hilo ambalo limewachukua wafua dhahabu 15 wiki mbili wakifanya kazi masaa 16 kwa siku kutengeneza na kuvisha shanga za dhahabu kwenye shati hilo.
"Nafahamu mimi si mwanaume mwenye mvuto duniani lakini hakika hakuna mwanamke atakayejizuia kuvutiwa na shati hili?" alifafanua.
"Shati la dhahabu imekuwa ni moja ya ndoto zangu," Phuge alilieleza gazeti la India la the Pune Mirror.
"Hii itakuwa kirembesho cha sifa yangu kama 'Mtu wa dhahabu ya Pimpri'", alisema Phuge.
Shati hilo lenye urembo mwingi liliundwa kutokana na kitambaa laini, na kuwekewa vifungo sita angavu na mkanda tatanishi, ambao pia umeundwa kwa dhahabu.